
Waziri wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizungumza wakati
alipofungua kikao cha wizara hiyo na wamiliki wa vyombo vya habari ili
kujadili na kuweka mkakati wa pamoja katika kuhamasisha watanzania
kujiandaa na kuingia katika utekelezaji sera ya serikali ya ujenzi wa
viwanda ili Tanzania iweze kufikia lengo la kuwa nchi ya uchumi wa
viwanda ifikapo mwaka 2020 kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Magazeti ya
serikali (TSN) Jim Yonaz na katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Profesa Elisante Ole Gabriel, Mkutano huo umefanyika kwenye ofisi za
wizara hiyo uwanja wa Taifa.

Mh. Nape Nnauye Waziri wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akimsikiliza Katibu Mkuu
wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel wakati akizungumza kumkaribisha Waziri huyo ili kuzungumza na
wadau wa vyombo vya habari katika kikao hicho kilichofanyika kwenye
ofisi za wizara hiyo Uwanja wa Taifa, kushoto ni Dk Jim Yonaz Mkurugenzi
wa TSN.

Mh. Nape Nnauye Waziri wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelelzo Dk. Hassan
Abbas wakati alipokuwa akitoa mada kwa wadau wa vyombo vya habari
kuhusu namna wadau hao wanavyoweza kushirikiana na serikali katika
kuhamasisha uwekezaji na ujenzi wa viwanda nchini.

Mhariri Mtendaji wa Gaseti la Jambo Leo Bw. Theophil Makunga akichangia hoja katika mkutano huo.

Mhariri Mtendaji wa ITV Bw. Steven Chuwa akichangia hoja katika mkutano huo

Baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari wakiwa katika mkutano huo.

Wadau mbalimbali wakifuatilia hoja mbalimbali katika mkutano huo.


Mh. Nape Nnauye Waziri wa Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakiwa
katika picha ya pamoja na wadau wa vyombo vya habari mara baada ya
kumalizika kwa mkutano huo leo.

SHARE
No comments:
Post a Comment