Makundi ya kutetea
haki za wanyama yamemlaumu rais wa Korea Kusini aliyeondoka madarakani
Park Geun-hye, kwa kuwatelekeza mbwa wake wakati aliondoka ikulu
Mzozo
huo unaibuka wakati Bi Park anaitwa kuhojiwa kufuatia kutajwa kama
mshukiwa kwenye sakata kubwa ya ufisadi ambayo ilichangia kuondolewa
kwake madarakani.- Rais wa Korea Kusini aondoka ikulu baada ya kutimuliwa madarakani
- Wabunge wapiga kura kumfuta rais wa Korea Kusini
Korea Kusini itafanya uchaguzi wake wa urais tarahe 9 mwezi Mei.
Bi Park ndiye rais wa kwanza aliyechagulia kidemokrasia kuondolewa madarakani.
Mwishoni mwa wiki Bi Park aliondoka ikulu ya rais ambayo inafahamika kam Cheong Wa Dae na kuelekea nyumbani kwake kwenye mtaa wa kifahari mjini Seoul.
Mbwa wake tisa hawakuwa miongoni kwa vitu alivyoandamana navyo.
Kundi la kupinga unyanyasaji wa wanyama linasema kuwa alikiuka haki za wanyama kwa kuwaacha nyuma.
Msemaji wa ikulu alikana madai kuwa Bi Park aliwatelekeza mbwa wake na kuliambia shirika la Reuters kuwa mbwa hao waliachwa nyuma kwa sababu haingekuwa vyema wao kuondolewa kwenye makazi yao.
"Aliwaambia wafanyakazi wa ikulu kuwa wawatunze mbwa hao na wawatafutia makao ikiwa itawezekana," msemaji wake alisema,
Bi Park alikuwa anawapenda mbwa wake, hadi wakapewa jina "mbwa kwa kwanza".
Korea Kusini imekuwa ikiongozwa na waziri mkuu Hwang Kyo-ahn tangu bunge lipige kura ya kumuondoa madarakani mwezi Disemba.
Tarehe ya uchaguzi wa rais ilitangazwa wakati wa mkutano wa mawaziri siku ya Jumatano
Wakati wa mkutano huo bwana Hwang alisema kuwa hatawania urais, hatua ambayo ilikuwa pigo kwa chama cha Conservative.
SHARE
No comments:
Post a Comment