Utafiti wa hivi karibuni umesema, wahudumu wa afya wapatao 800
wameuawa kutokana na vitendo vya uhalifu wa kivita nchini Syria tokea
mwaka 2011, ikiwa ni pamoja na ulipuaji wa mabomu katika hospitali
mbalimbali, mauaji ya riasasi, mateso, ambayo yote yanatajwa kufanywa na
vikosi vinavyoungwa mkono na serikali. Kulingana na uchambuzi
uliochapishwa katika jarida la matibabu The Lancet, serikali ya Syria
pamoja na mshirika wake mkuu Urusi, wanazuia huduma ya afya na kuitumia
kama silaha ya vita. Ripoti hiyo imeandikwa kwa ushirikiano wa wataalamu
wa vyuo vikuu vya Beirut, Uingereza, Marekani pamoja na jumuiya ya
matibabu ya Syria na Marekani (SAMS) pamoja na Shirika liliso la
Kiserikali la Multi-Aid Programs. Jarida la The Lancet limelitolea wito
Shirika la Afya Duniani WHO kukusanya fedha za kuimarisha miundombinu ya
afya nchini Syria na kuhamasisha misaada zaidi ili kukomesha mgogoro
huo wa kibinaadamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment