Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye amezipongeza Kurugenzi za
Mawasiliano Ikulu na Idara ya Habari MAELEZO kwa ubunifu wanaouonesha
katika kuelezezea mafanikio ya Serikali kwa kutumia teknolojia
mbalimbali za habari na mawasiliano.
Waziri
Nape alisema licha ya changamoto ya vifaa vinavyowakabili Maafisa
Mawasiliano wa Serikali wamekuwa wanafanya kazi nzuri za kuisaidia
Sarikali ,amewataka kuwa wabunifu kwa kutumia teknolojia ya habari na
mawasiliano hasa mitandao ya kijamii katika kutekeleza majukumu yao
kwani ni nafuu na rahisi.“Nawapongeza wakurugenzi vijana Dkt. Hassan
Abbasi wa MAELEZO na Grayson Msigwa wa Ikulu, hawa ni mfano wa ubunifu
wa namna Serikali inavyoweza kutumia teknolojia mbalimbali za
mawasiliano katika kuhakikisha mazuri yanayofanywa na Serikali
yanatangazwa, yanaenezwa na kutetewa”alisema Waziri Nape.
Waziri
Nape aliongeza kuwa pamoja na ubunifu wao katika mitandao ya kijamii,
utayarishaji wa makala za Serikali na kujibu hoja kwa haraka kupitia
taarifa kwa umma, wameweza pia kubuni vipindi vya TUNATEKELEZA na SAFARI
YA DODOMA ikiwa ni mkakati wa kusukuma mbele ajenda za Serikali.Aidha,
Waziri Nape amewataka Maafisa Mawasiliano kutumia fursa zinazotolewa na
baadhi ya vyombo vya habari binafsi kupitia vipindi vya bure kwenye
Televisheni, redio na magazeti kuhakikisha mambo mazuri yanayotekelezwa
na Serikali yanatangazwa na kuweza kusikika kwa Wananchi.“Nimezungumzia
hoja na haja ya mabadiliko kiutendaji, lakini nikiwa kiongozi ambaye pia
katika maisha yangu nimefanya kazi ya kuongoza kitengo cha habari na
uenezi nafahamu changamoto zinazoikabili kada hii,lakini unaweza
ukageuza changamoto kuwa fursa,kwahiyo tujiongeze ndugu zangu ” alisema
Waziri Nape.
Waziri
Nape alitoa wito kwa Makatibu Wakuu, Wakurugenzi,Wakuu wa Taasisi pamoja
na watendaji wakuu katika ofisi za umma kuhakikisha wanatenga fedha
katika bajeti kwaajili ya kununua vifaa vya kutendea kazi ili
kuviwezesha vitengo vya Mawasiliano Serikalini kutekeleza majukumu yake
kwa ufasaha na ufanisi katika kuisemea Serikali.
SHARE
No comments:
Post a Comment