Mtoto
wa Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Ridhiwani Kikwete
amesema ameshahojiwa na kamisheni ya kupambana na dawa za kulevya na
kukutwa hana hatia kuhusu tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya
dawa za kulevya iliyokuwa ikimkabili.
Mbunge
huyo wa Jimbo la Chalinze ambaye pia ni mwanasheria, jina lake
lilitajwa kwenye list ya majina 97 ya watuhumiwa wa biashara haramu ya
dawa za kulevya ambayo RC Makonda aliikabidhi kwa Kamishna wa kupambana
na dawa za kulevya nchini, Rogers Sianga kwajili ya mahojiano.
Katika
taarifa yake aliyoitoa Jumanne hii, Ridhiwani amesema ameshukuru kuona
haki imetendeka katika sakata hilo lililokuwa likimkabili.
“Ni
kweli niliitwa na kuhojiwa. Serikali yangu chini ya Kamisheni ya Madawa
ya kulevya inasimamia haki na nimeona ikitendeka. Niko huru toka kwenye
tuhuma/kashfa,” Ridhiwani aliandika Instagram.
Aliongeza,
“Tuunge mkono juhudi hizi. Tuunge mkono hatua zinazochukuliwa ili
kuokoa vijana wetu na kulinda nguvu kazi ya Taifa #vitadhidiyaMadawa
#magufulinikazitu #tanzaniakwanza #miminikazitu #chalinzenikazitu,”
Alisema
hiyo ni taarifa yake ya mwanzo kwa kuwa amebanwa na majukumu ya kazi na
ukifika wakati atoa taarifa rasmi kuhusu sakata hilo.
SHARE
No comments:
Post a Comment