TRA

TRA

Monday, April 3, 2017

ASKOFU DKT NDALIMA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUZIDI KUMUOMBEA RAIS DKT MAGUFULI AWAONYA WANAOGEUZA MAKANISA MAJUKWAA YA SIASA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


DSC_0031
Askofu  wa  kanisa la Pentecote Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt
Rejoice Ndalima akifaya maombi
Baadhi ya  waumini  wa kanisa hilo
mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Iringa Paul Mtakwimwa
Askofu  wa kanisa la Pentecoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt
Rejoice Ndalimaakiwaombea  waumini wake na Taifa
Wachungaji wakiwa katika maombi
Askofu  wa kanisa la Pentecoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt
Rejoice Ndalima akimsimika mchungaji Paul Mtakimwa na mkewe
Waumini  wakiwa katika maombi maalum
Na MatukiodaimaBlog
ASKOFU  mkuu  wa kanisa la Pentecote  Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania  Dkt
Rejoice Ndalima  amewataka  viongozi wa
dini  nchini  kutumia nyumba  za ibada  kumwombea Rais Dkt John Magufuli na  kuliombea Taifa badala ya kutumia nyumba  hizo kusema kuumbua viongozi
wa  serikali .
Kuwa kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Magufuli katika  nchi
hii si  ya kubenzwa makanisani na
wachunguzaji ama viongozi wengine wa
dini bali ni kazi ambayo inapaswa
kuombewa  zaidi  ili
Taifa  lizidi kubarikiwa .
Askofu  huyo ametoa
kauli hiyo jana  wakati wa  uzinduzi wa kanisa hilo  Mtwivila
mjini Iringa pamoja na kumsimika mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Paul
Mtakwimwa   ,kuwa hivi  sasa
heshima ya  nyumba  za ibada
imeanza kupoteza uwepo  wa Mungu
kutokana na baadhi ya  watu  kutumia
nyumba   za  ibada kama
sehemu ya masengenyo na utapeli jambo
ambalo  si  sahihi .
Alisema  kitendo  cha baadhi ya makanisa nchini kutumiwa na
wanasiasa ama vikundi vya  watu  kuishambulia serikali ama  kufanya utapeli  wa fedha
za  waumini wao kwa kuwatoza fedha  kama malipo ya huduma  wanayoitoa si
sahihi na si kazi ya  nyumba  za ibada hasa makanisa .
Pasipo  kutaja majina
ya makanisa   yaliyogeuzwa majukwaa ya
wanasiasa na baadhi ya  watu  waovu ama yanayofanya utapeli  wa
pesa  kwa  waumini
wake ,alisema  kuwa yamezuka
makanisa ambayo kimsingi hayakupaswa
kuitwa makanisa  ili yalipaswa
kuwa ni vyama  vya siasa ama nyumba  za
waganga  wa  kienyeji kwa maana ya  wapiga ramli .
“ Baadhi ya makanisa
yamepoteza sifa ya  kuitwa ni
makanisa maana  wanafanya  vituko vya ajabu sana  ndani ya madhabahu ya Mungu …wapo  wanaotumiwa na wanasiasa  kueneza siasa makanisani na  kila
siku  wao ni kuwa ni
wachonganishi  dhidi ya  serikali na
watu wake na wengine wamegeuka
watabiri wa  uongo na watenda
miujuzi hatarishi kwa jamii “
Alisema  kuwa kazi ya
viongozi wa  dini  ni
kuhubiri  neon ili  watu  wote  waweze kumjua Mungu na  sio kuhubiri siasa ama  kuifundisha kazi serikali ya  kufanywa wakati si  jukumu la kanisa kuwa  iwapo watu
wote  watamjua  Mungu
watafanya kazi ya kuhudumia
jamii  kwa  kutanguliza
hofu ya  Mungu hivyo  hakutakuwa na ufisadi , wizi ama
watumishi  hewa hivyo kazi ya kanisa ni
kuwafanya watu waijue kweli na kweli  iwe
ndani ya  mioyo yao.
Askofu Dkt   Ndalima
alisema kuwa kanisa   lake  limeenea
nchi nzima na katika mkoa  wa
Iringa  wameanzisha makanisa mawili  katika
mji  wa Iringa na Nyololo  wilaya ya
Mufindi ila lengo lao ni  kuhubiri
neon la Mungu kwa usahihi na kuepuka kuwa
kanisa la ujanja ujanja  kama  wanavyofanywa baadhi ya  watu
wanaojiita manabii  ila kazi
wanayoifanya  ni  sawa na manabii  wa uongo .
Akielezea  kuhusu
utendaji kazi wa Rais  Dkt  Magufuli askofu  huyo
alisema kanisa lake  linampongeza
kwani hivi sasa nchi imekuwa na utulivu mkubwa na hakuna  tena maandamano ya  vurugu na
kuwa kila wakati makanisa  yake
yatatenga mudu  wa  kumuombea Rais na  watendaji
wote wa serikali na kutumia Biblia katika ibada  zake na
sio  kutumia  matukio na kashfa  za
viongozi  kuhubiri kanisani .
MWISHO

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger