Timu ya taifa ya Tenisi ya watu
wenye ulemavu inahitaji msada mkubwa wa fedha na vifaa ili kuhakikisha
wanashiriki vyema mashindano ya dunia ya BNP Paribas World Team
yatakayofanyika nchini Itali kuanzia tarehe moja ya mwezi wa tano hadi
tarehe saba mwaka huu.
Mwenyekiti wa chama cha Tenisi
Tanzania,Dennis Makoi alisema kwamba kwa sasa washiriki wanaendelea
vyema na maandalizi lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya vifaa
ambavyo vitawawezesha kushiriki vyema mashindano hayo.
Makoi alisema kwamba kiujumla
hali maandalizi kwa upande yako vizuri kwani wachezaji wanaendelea vyema
na mazoezi ili kuweza kufanikisha wanafanya vyema kwenye mashindano kwa
kuipeperusha vyema bendera ya Taifa na Afrika kwa ujumla.
Nae kocha mkuu wa timu hiyo
Riziki Salum alisema kwamba kikosi chake kinataraji kuanza safari siku
ya tarehe 29 ya mwezi huu ikiwa na jumla ya wachezaji 4.
Riziki alisema kwamba bado
msafara huo unakabiliwa na changamoto kubwa katika upande wa
tiketi,hivyo ni vyema wadau na makampuni kujitokeza kuisaidia timu hiyo
ya Taifa ya mchezo wa Tenisi kwa watu wenye ulemavu.
SHARE
No comments:
Post a Comment