BABA Mtakatifu Fransisko amemteua Askofu Mkuu Marek Solczyński kuwa
Balozi mpya wa Vatikani nchini Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Mkuu
Solczyński alikuwa Balozi wa Vatikani nchini Georgia, Armenia na Azerbaijan.
Itakumbukwa kwamba, Askofu Mkuu
Solczyński alizaliwa Aprili 7, 1961 huko Stawiszyn, nchini Poland. Baada ya
masomo na majiundo yake ya Kikasisi, mnamo Mei 28, 1987 akapewa Daraja Takatifu
ya Upadri.
Baada ya kufanya utume wake katika masuala ya diplomasia sehemu mbali mbali, tarehe 26 Novemba 2011, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu Mkuu na kumwekwa wakfu tarehe 6 Januari 2012. Askofu mkuu Marek Solczyński ameshiriki kikamilifu katika maandalizi ya hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Fransisko nchini Georgia, Armenia na Azerbaijan aliyoitekeleza mwaka 2016.
SHARE
No comments:
Post a Comment