Wataalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu
cha Penn State, Marekani wamegundua katika utafiti wao kuwa zaidi ya 90%
ya watoto waliopitia maisha ya kunyanyaswa, kupigwa au kudhalilishwa
kingono wanabalehe haraka ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa
upendo.
Professor Jennie Noll aliliambia Jarida la Adolescent Health: >>> “Watoto
hasa wa kike wanaolelewa kwa kunyanyawa hasa kupigwa au kubakwa
hubalehe kabla ya muda ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa upendo
pia watoto wa aina hii huota matiti mapema ukilinganisha na watoto wa
kawaida.“
Akielezea
uhusiano ulipo baina ya mtoto kunyanyaswa na kubalehe kabla ya wakati
Dr. Noll alisema watoto wanaokuwa katika mazingira kama hayo huzalisha
homoni nyingi zinazotokana na msongo mkubwa wa mawazo hivyo kuharakisha
muda wa balehe.
Wanasaikolojia
hao pia walisema mtoto anayenyanyaswa yuko hatarini zaidi kupata
saratani ya ovari na matiti ukilinganisha na watoto ambao hulelewa
kwenye mazingira ya upendo na amani.
SHARE
No comments:
Post a Comment