TRA

TRA

Sunday, April 23, 2017

MAREKANI VS KOREA KASKAZINI; APRILI 25, 2017 KUAMUA KAMA VITA IPO AU LA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Kombora la kinyuklia likiwa limebebwa na gari la kijeshi


NA K-VIS BLOG NA MASHIRIKA YA HABARI, SEOUL/BEIJING/RUSSIA
WIZARA ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini imetoa taarifa ikisema Jeshi la Wananchi wa Korea Kaskazini, (KPA), litajibiza kwa nguvu kubwa uvamizi wowote utakaofanywa na Marekani.
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim
"Kwa sasa tumeweka nguvu za kinyuklia kujilinda wenyewe kutokana na vitisho vya silaha za kinyuklia za Marekani. Tutajibu bila kusita hata kidogo na tutajibu vita kwa vita, nyuklia kwa mtindo wetu wa mashambulizi ya kinyuklia na tuna hakika tutaibuka washindi mwisho wa mapambano yetu na Marekani.” Taarifa hiyo ilisema.
Korea Kaskazini inatarajiwa kuadhimisha miaka 85 ya kuanzishwa kwa misingi ya Jeshi la Wananchi wa Korea, (KPA), Jumanne Aprili 25, 2017, ambapo maadhimisho hayo yanakamilisha mazoezi ya kijeshi wakati wa majira ya baridi. Wakati huo huo Marekani na Korea Kusini, wanaendelea kufanya mazoezi ya pamoja yataendelea hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Aprili. Msemaji wa Wizara ya Muungano Muungano wa Serikali ya Seoul, Lee Duk-haeng, amesema.
“Ni hali ya kutapakaa kwa mazoezi ya vifaa vya kijeshi Korea Kaskazini na maandalizi ya kimkakati ya vifaa hivyo imeelekezwa kwenye Rasi ya Korea (Korean Peninsula), kwa sababu ya mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya Korea Kusini na Marekani.” Alisema Lee.
Manowari ya kubeba ndege ya Marekani US Carl Vinson
Kwa haraka haraka vita hii itayavutia au kuyahusisha mataifa sita, kwa upande mmoja, Marekani ina washirika wake ambao ni Korea Kaskazini, na Japan, ambao wote ni majirani na Korea Kaskazini, huku kwa upande mwingine, Korea Kaskazini inaungwa mkono na China na Russia.
Naye Rais wa Marekani amlisema Alhamisi iliyopita kuwa “mienendo isiyo ya kawaida imekuwa ikijionyesha katika masaa mawili au matatu. Alisema anaimani na Rais wa China Xi Jinping “atajaribu kwa nguvu kubwa” kuwashinikiza Korea Kaskazini kuhusu nyuklia na mipango yake ya makombora.
Rais Trump na Rais Xi
Hat hivyo Trump hakuonyesha mienendo hiyo ina maanisha nini, na hakuna afisa yeyote wa Marekani aliyeliambia Sirika la Habari la Uingereza Reuters, kuhusu kupanda kwa joto la harakati za kijeshi za Makombora ya China yakiashiria kuwa wanajua kwa usahihi sababu za miendendo hiyo.
Rais Trump aliandika kwenye Tweeter yake kuwa “China ni msaidizi mkuu wa kiuchumi wa Korea Kaskazini, wakati kutokuwa na kitu si rahisi, kama wanataka kutatua suala la Korea Kaskazini wanaweza.” Aliandika.
Wizara ya Ulinzi ya China imesema, majeshi yake yaliyoko kwenye mpaka wake na Korea Kaskazini, yalikuwa yanajiimarisha katika hali ya kawaida ya kujiweka tayari kijeshi na mafunzo.
Alipotakiwa kuzungumzia tweet hiyo ya Trump, Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Lu Kang alisema, Rais Xi na Trump walikuwa na majadiliano mapana kuhusu Korea Kaskazini, walipokutana mwezi nchini Marekani.
Fukuto la kutokea kwa vita kwenye Rasi ya Korea, linazidi kushika kasi huku Korea Kusini ikisogeza vifaa vyake vya kijeshi kwenye kona zote za mpaka wake na Korea Kaskazini Ijumaa Aprili 21, 2017.
Tayari Marekani ambayo inatajwa kuwa ndiyo kinara wa “vita” hiyo, imekwisha sogeza meli yake ya kubeba ndege, Carl Vinson kwenye Rasi ya Korea.
Joto hilo la vita litazidi kupanda zaidi, Aprili 25, ambapo Pyongyang inatarajiwa kufanya sherehe kubwa zaidi ya kijeshi ambapo tayari Korea Kaskazini imetishia kufanya jaribio linguine la Kinyuklia.
 “Tunafuatilia kwa karibu hali ya mambo, alisema na kuongea Korea Kusini haiwezi kuacha ulinzi wake ukianguka.
Korea Kaskazini imesema Ijumaa kuwa hali ni tete na hatari kwenye Rasi ya Korea kwa sababu ya upuuzi (madcap) wa Marekani wa kutumia vita vya Kinyuklia kwa lengo la kuingilia utawala wan chi hiyo na haki ya kuishi.”
Hali ilizii kuwa tete kwenye miezi ya hivi karibuni baada ya Korea Kaskazini kufanya majaribio mawili ya makombora ya kinyuklia mwaka jana na kufanya jaribio lingine la kombora la masafa marefu, (Intercontinental ballistic missile).
Rais wa Marekani, Donald Trump ameapa kuizuia Korea Kaskazini kuwa na uwezo wa kuipiga Marekani kwa bomu la nyuklia.
Kaimu Rais wa Korea Kusini, President Hwang Kyo-ahn amewaambia maafisa wa juu wa serikali yake kuwa kuna shaka maadhimisho ya miaka 85 ya misingi ya jeshi la Korea Kaskazini hapo Aprili 25, yakatumika kufanya uchokozi tena.
Vifaru vya Korea Kusini
Picha mpya za Satalaiti zinazochambua 38North, mradi wa kuratibu masuala ya Korea Kaskazini wenye makazi yake mjini Washington Marekani umeona harakati za kijeshi zikiendelea huko Korea Kaskazini kwenye eneo la kufanya majaribio ya kinyuklia la Punggye-ri. Lakini wachambuzi hao hawaksuema kama harakati hizo kuelekea jaribio linguine.
“Kando na picha hizo za satalaiti kuendelea kuonyesha harakati hizo za kijeshi, inaonyesha kuwa eneo hilo la Pungyang-ri, huenda likatumika kufanya jaribio la sita la kombora la inyuklia.” 38North imesema katika uchambuzi wake Ijumaa Aprili 21, 2017.
Maafisa wa Marekani pia wamesema, kumekuwepo na hali isiyo ya kawaida kwa Wafyatua makombora wa China hali inayoashiria kujiweka tayari kufuatia mshirika wake mkubwa aliyetengwa, Korea Kaskazini kuzongwa na matishio ya vita. Hata hivyo maafisa wa China wamepuuzia taarifa hizo na kukanusha taarifa kuwa ndege zake za kijeshi zimewekwa tayari.
Jeshi la Russia nalo limekanusha taarifa za vyombo vya habari Ijumaa iliyopita kuwa lilikuwa likiviandaa vikosi vyake kwenye mpaka wake na Korea Kaskazini, Shirika la habari la Ruassia Interfax limesema, likimnukuu msemaji wa jeshi la Russia.
 Hwang Kyo-ah(kulia) na Tillerson            
“Moscow imesema, mienendo ya kijeshi inayoonwa na wananchi kwenye maeneo hayo ni ya kawaida na ilkuwa imepanwga kabla ya sekeseke la sasa.”
Habari za hivi punde zinasema Korea Kusini imetangaza kuwa  raia wa Marekani ametiwa mbaroni na maafisa wa usalama wa Korea Kaskazini, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pyongrang Aprili 23, 2017.
Huyu ni mtu wa tatu kutoka Marekani kukamatwa na maafisa wa serikali wa Korea.
Mmarekani huyo mwenye asili ya Korea Kaskazini alikuwa anajiandaa kupanda ndege kurejea Marekani, na kwamba alikuwa nchini humo kujadili masuala ya misada.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger