TRA

TRA

Wednesday, May 31, 2017

WANAHABARI, WATAFITI WA KILIMO KUTOKA NCHI TANO ZA AFRIKA WAAGANA HOTELI YA MALAIKA BEACH RESORT JIJINI MWANZA

No comments:
 Mwanahabari Lucy Ngowi (kushoto), akichangamkia mapochopocho katika hafla ya kuagana kati ya wanahabari kutoka nchi tano za Afrika na wataalamu wa kilimo kutoka katika nchi hizo baada ya kumaliza ziara ya utoaji wa mafunzo kwa maofisa ugani wa Wilaya ya Chato mkoani Geita na Buchosa Sengerema hafla iliyofanyika Hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza jana usiku. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Jukwaa la Bioteknolojia Afrika (OFAB) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti na Maendeleo kwa ajili ya Manufaa ya Wakulima Wadogo (AATF). Kutoka kulia ni Ofisa kutoka idara ya Fedha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mr Nyamka na dereva wa Costech Mr. Nasibu.
Read more »

MBUGA ZA WANYAMA UNAZOWEZA KUTEMBELEA BURE WIKENDI HII?

No comments:
Na Jumia Travel Tanzania

Siku ya Jumatatu ya Juni 5 itakuwa ni maadhimisho ya ‘Siku ya Mazingira Duniani’ ambayo huadhimishwa na mataifa tofauti duniani ikiwa imebeba kauli mbiu ya ‘Kuwaunganisha Watu na Mazingira Asilia.’ 

Mapema wiki hii Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba  alitoa taarifa kwa umma kuwa kwa hapa nchini maadhimisho ya siku hiyo kitaifa yatafanyika kijijini Butiama mkoani Mara, mahali alipozaliwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl. Julius Nyerere, ikiwa ni kuenzi jitihada zake za kulinda na kuhifadhi mazingira.
Read more »

No comments:
wandishi Wetu


KAMPUNI ya bima ya Britam-Tanzania imezindua bima ya afya inayolenga kuhudumia makampuni makubwa, biashara ndogo na za kati (SMEs).
 
Bima hii inajumuisha gharama za matibabu ya wagonjwa waliolazwa, vipimo vya magonjwa mbalimbali pamoja na majeraha yaliyotokana na ajali kwa waajiriwa wasiopungua 10. Bima hii itagharimu kati ya shilingi milioni 5 mpaka milioni 200.
 
Akiongea katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo,Steven Lokonyo alisema bima hii itagharamia kumsafirisha mgonjwa mahututi mpaka hosipitali, ushauri wa daktari, gharama za chumba maalumu cha uangalizi (ICU), mazoezi ya viungo, tiba ya mionzi, pamoja gharama za upasuaji.
 
Pia bima hii itagharamia kumsafirisha mgonjwa mahututi kwa ndege au gari kwenda hosipitali kupata huduma za matibabu, gharama za uchunguzi za eksirei na uchunguzi wa  kimaabara.  
 
"Bidhaa hii tunayoileta kwenye soko inakuja kuleta mabadiliko katika sekta ya afya na itaenda mbali kusaidia biashara ndogo na za kati na makampuni makubwa hivyo kukuza ustawi pamoja na uzalishaji wa wafanyakazi wao" alisema Lokonyo.

Lokonyo alibainisha pia kwamba bima hiyo ina faida za nyongeza kama vile tiba ya ugonjwa sugu uliogunduliwa, magonjwa ambayo mtu anayo kabla ya kuanza kutumia bima,UKIMWI na magonjwa mengine kama kisukari, kansa, magonjwa ya figo, ukurutu, maumivu ya viungo, magonjwa ya ini na kadhalika.

Uzinduzi wa bima hiyo umefanyika kwa kuzingatia uhitaji wa soko pia ni mkakati wa kampuni kupanua biashara yake ya bima nchini kwa kuangalia makundi ya watu ambayo yalikuwa hayajafikiwa na huduma za bima.

"Bima hii imeanzinduliwa kwa kuangalia uhitaji wa biashara ndogo na za kati pamoja na makampuni. Kampuni yenye wafanyakazi 10 sasa inaweza kupata huduma ya bima ambayo kila mtu anajua afya ya wafanyakzi ni muhimu kwa biashara yoyoye" aliongeza Lokonyo.
 
Takwimu za hivi karibuni zimeonyesha kuwa matumizi ya bima nchini Tanzania ni chini ya asilimia moja ya pato la taifa ambacho ni kiwango cha chini ukilinganisha na nchi zilizoendelea na nchi nyingine nyingi za kiafrika. Katika jitihada zake za kufikia watanzania wengi zaidi, Britam inapanua matawi yake nchini ambapo kwa sasa wapo katika mikoa saba ya Dar-es-salaam, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Mtwara, na Arusha.
 
Kampuni ya bima ya Britam Tanzania amabayo ilijulikana kama kama 'Real Insurance' hapo mwanzo ni kampuni tanzu ya 'Britam Holdings' ambayo inatoa huduma mbalimbali za kifedha katika bima, usimamizi wa mali, na benki.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam-Tanzania, Stephen Lokonyo akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, wakati wa uzinduzi wa bima ya afya hapa nchini. Katikati ni Mkuu wa Bima ya Afya ya kampuni hiyo, Christine Mungi na kulia ni Mkuu wa Fedha na Utawala, Irene Godson. (NA MPIGA PICHA WETU)

TGNP YAWANOA MADIWANI DAR KUHUSU UONGOZI WA KIJINSIA

No comments:

Grace Kisetu, Mkuu wa Idara ya Ijenzi wa Nguvu Pamoja wa TGNP Mtandao, akizungumza na washiriki katika warsha ya Uongozi wa Kijinsia kwa Madiwani wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Read more »

Mifupa ya gwiji wa Brazil Garrincha haijulikani ilipo

No comments:


Vyombo vya habari nchini Brazil vinasema kuwa mifupa ya gwiji wa zamani wa soka nchini humo Manuel Francisco dos Santos maarufu kama Garrincha, inaweza kuwa imepotea zaidi ya miongo mitatu baada ya kifo chake akiwa na miaka 49.


 Garrincha (kushoto) na Pele walitengeneza safu hatari ya ushambuliaji Brazil

Kuna makaburi mawili ambayo yote yana majina yakemjini Rio de Janeiro lakini inawezekana kati ya hayo hakuna hata moja ambalo ni lake. 

Mmoja wa wahifadhi wa makaburi hayo anasma kuwa mifupa yake inaweza kuwa ilihamishwa miaka kadhaa iliyopita ila haijulikani wapi haswa ilipelekwa.

Garrincha mpinzani mkubwa wa Pele wa ni nani zaidi katika historia ya soka kwa nchi hiyo,aliisaidia nchi yake kutwaa kombe la dunia mwaka 1958 na 1962.

Wenger ashauriwa kuwauza Sanchez na Ozil

No comments:


Mlinzi wa zamani wa klabu ya Arsenal Martin Keown amesema kuwa meneja wa Klabu hiyo Arsene Wenger anapaswa kuwauza nyota wake Alexis Sanchez na Mesut Ozil baada ya kuongeza muda wa kusalia kinoa miamba hiyo ya London.

Mfaransa huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na amesema kuwa timu yake inaweza kupigana na kutwaa ubingwa msimu ujao.
Viungo Alexis Sanchez na Mesut Ozil kwa pamoja wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa mwaka huu.


 Kwa pamoja Sanchez na Ozil wamekuwa nguzo muhimu kwa klabu ya Arsenal

Kewon anasema kuliko kupata hasara ya kuwaruhusu kuondoka bure ni vyema akafanya maamuzi magumu ya kuwauza nyota hao na kutengeneza faida itakayoweza kuleta wachezaji wapya na wenye morali kubwa zaidi. 

Sanchez amefunga magoli 24 na kuchangia kupatikana kwa mengine 10 huku Ozil akifunga nane na kuchangia tisa lakini hiyo haikutosha kuifanya timu hiyo kukosa michuano ya mabingwa wa Ulaya msimu ujao jambo ambalo linatia ukakasi kwa Sanchez na Ozil kuongeza mikataba yao.

Sanchez amepewa ofa ya paundi 300,000 kwa wiki lakini bado hajasaini mkataba huo, huku Ozil akikataa paundi 250,000 kwa wiki.

Taifa Stars yaanza kambi nchini Misri

No comments:


Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania inatarajiwa kuanza mazoezi yake usiku huu baada ya kufika salama mjini Alexandria,nchi Misri kwa ajili ya kuweka kambi.

Akizungumza mara baada ya kukagua viwanja vya mazoezi leo asubuhi, Kocha Mayanga ambaye alipewa majukumu ya kuifundisha timu hiyo mapema - Januari, mwaka huu, amesema: 

"Programu ya mazoezi kwa timu hii itaanza leo saa 2.00 usiku. Ingawa siku nyingine nitafanya asubuhi na jioni."

 Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga upande wa kulia akiwa na wasaidizi wake wakikagua Uwanja ambao utautumia kwa ajili ya mazoezi kwenye kambi ya Tolip Sports City, Alexandia, Misri.

Taifa Stars inayopiga kambi hapa Misri, inajiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku.

Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi 'L' kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika NCHINI Cameroon.
Mbali ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi 'L' ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo.

WEWE ENDELEA KULAUMU TU, WENGER ANAENDELEA KUCHOTA MAMILIONI ARSENAL

No comments:





Pamoja na mashabiki wengi wa Arsenal kuonekana wangependa Arsene Wenger aondoke, yeye ameendelea kuchota mamilioni.

Tokea atue Arsenal, Kocha Arsene Wenger amechota takribani Sh pauni milioni 40 kwa ajili ya usajili wake tu.

Mara ya kwanza mwaka 1996 alipojiunga na Arsenal akitokea Japan, Wenger alilipwa pauni 500,000. Lakini mkataba wake mpya wa miaka miwili atalipwa pauni milioni 8.

Hii inamfanya Wenger kuwa katika kundi la makocha watano wenye thamani ya juu katika ligi hiyo kila wakati wa kusaini mkataba mpya.

MISHAHARA JANGWANI YAFIKIA MIEZI MINNE, WACHEZAJI WALIA CHINICHINI

No comments:




Bundi wa maisha magumu ameendelea kuzunguka katika mitaa ya Jangwani baada ya wachezaji wake kuanza kulalama chinichini kwamba mshahara sasa umefikia miezi minne.

Wachezaji wa Yanga hawajalipwa mishahara ya miezi minne sasa, jambo ambalo limewafanya waanze kulalamika.

"Kabla ya kwisha kwa ligi, tuliambiwa tupambane kubeba ubingwa. Mambo yatakuwa safi, lakini naona hali si nzuri hadi sasa. 

"Mwisho wa mwezi huu (Mei), itakuwa miezi minne. Mmekuwa mkisema hatujitumi, hatuvumilii. Basi sasa mtutetee, maana miezi minne mingi ndugu zangu na sisi tuna familia," alisema mmoja wa wachezaji wa Yanga.

Viongozi wa Yanga wamekuwa wakikubali kwamba mishahara imekuwa tabu na baada ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wao, Yusuf Manji, mambo yamezidi kuwa mabaya zaidi.

Wachezaji hao walipambana mwishoni bila ya mishahara hadi kufanikiwa kufikisha pointi 68 zilizowapa ubingwa kwa tofauti ya mabao dhidi ya Simba.

MAJALIWA ATEMBELEA MAONYESHO YA UJENZI WA NYUMBA

No comments:


unnamed
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama picha za nyumba wakati alipotembelea Maonyesho ya Mpango wa ujenzi wa Nyumba za Gharama Nafuu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma  Mei 30, 2017. Maonyesho hayo yameandaliwa na Muungano wa  Vikundi Vya Vicoba Tanzania (VIGUTA) .Kushoto  ni  Mwenyekiti wa Taifa wa VIGUTA, Dkt. Salmin Ibrahim Dauda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UNICEF NA UNHCR WATOA ELIMU KUHUSU HAKI ZA WATOTO WAKIMBIZI MKOANI KIGOMA.

No comments:


unnamed
Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto Duniani (UNICEF) Bibi. Stephenie Shanler akizungumza na washiriki wa mkutano maalum (hawapo pichani) wa  utoaji elimu juu ya Haki za watoto wakimbizi unaoendelea kwa siku mbili mkoani Kigoma.
2
 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi Duniani (UNICEF) Bw. Raymond Chikwanda  akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutano maalum(hawapo pichani)  wa utoaji  elimu juu ya Haki za watoto wakimbizi unaoendelea kwa siku mbili mkoani Kigoma.
4
Kamishna wa Ustawi wa Jamii  Bw. Rabikira Mushi akizungumza katika mkutano maalum ulioandaliwa na UNICEF na UNHCR kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu Haki za watoto wakimbizi kwa washiriki kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto,Wizara ya Mamboya Ndani, Ofisi ya Waziri Mkuu, na Taasisi na Mashirika yanayotetea Haki za Watoto nchini leo Mei 31,2017 mkoani Kigoma.
3
 Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw.Darius Damas  akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutano maalum(hawapo pichani)  wa utoaji elimu juu ya Haki za watoto wakimbizi unaoendelea kwa siku mbili mkoani Kigoma.
5
 Baadhi ya washiriki kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ,Wizara ya Mamboya Ndani, Ofisi ya Waziri Mkuu, na Taasisi na Mashirika yanayotetea Haki za Watoto nchini wakifuatilia mkutano maalum wa utoaji elimu juu ya  Haki za watoto wakimbizi  unaofanyika  mkoani Kigoma.
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kifo cha Philemon Ndesamburo

No comments:


WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, PROF. JUMANNE MAGHEMBE AFANYA MAZUNGUMZO LEO NA BALOZI WA CHINA NCHINI, DKT. LU YOUGING, MJINI DODOMA

No comments:


Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing ofisini kwake mjini Dodoma ambapo wamejadili na kukubaliana mambo mbali mbali ya kuimarisha uhusiano wa China na Tanzania katika sekta ya maliasili na utalii. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kuwakaribisha wawekezaji katika sekta ya viwanda vya uchakataji wa mazao ya misitu na ujenzi wa hoteli katika fukwe za Tanzania na Hifadhi za Taifa.
 Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing akimueleza jambo Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma jana. Balozi huyo amekubali ombi la Waziri Maghembe kuwaleta wadau wa mashirika ya utalii kutoka nchini China kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania na kuvitangaza nchi kwao.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimfafanulia jambo balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing alipomtembelea ofisi kwake jana mjini Dodoma. Waziri Maghembe kupitia balozi huyo ameipongeza Serikali ya China na Wananchi wake kwa uamuzi wake wa hivi karibuni wa kufungia biashara haramu ya meno ya tembo nchini humo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiagana na Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing baada ya mazungumzo marefu ofisini kwake leo mjini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia), Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing (kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Justa Nyange wakijadili jambo muda mfupi baada ya mazungumzo hayo. (PICHA ZOTE NA HAMZA TEMBA - WMU)

Dkt. Yamungu Kayandabila na Dkt. Bernard Kibese wateuliwa kuwa Naibu magavana benki kuu ya Tanzania

No comments:


DKT. NCHIMBI AAGIZA HALMASHAURI KUANZISHA BENKI ZA WANA MICHEZI NA KUTENGA VIWANJA VVYA MICHEZO MKOANI SINGIDA.

No comments:


Halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida zimeagizwa kutenga maeneo yenye hadhi ya kuwa viwanja vya michezo pamoja na kuhakikisha zinakuwa na benki ya wanamichezo katika halmashauri zao.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa maagizo hayo leo asubuhi kabla ya kuzindua mashindano ya michezo kwa shule za Sekondari (UMISSETA) kwa ngazi ya mkoa ambapo wanamichezo hao wataunda timu za Mkoa kwa ajili ya mashindano ya kitaifa yatakayofanyika jijini Mwanza mwezi ujao.

Dkt. Nchimbi amesema halmashauri zimekuwa zikiwatelekeza wanamichezo mahiri hivyo wakianzisha benki ya wanamichezo kwa maana ya kuhifadhi kumbukumbu za wana michezo mahiri pamoja na kuwaendeleza hawatapata shida kipindi cha mashindano yoyote. 

Ameongeza kuwa halmashauri zimekuwa zikijisahau katika kuandaa maeneno ya michezo hadi inapofika kipindi cha UMISETA hali inayopelekea kukosekana kwa viwanja vya kufanyia mazoezi ili kuwa na timu bora.

Dkt. Nchimbi amewaasa wana michezo kuwa na nidhamu, utii, bidii na kuitumia michezo kuutangaza Mkoa wa Singida wenye fursa nyingi za uwekezaji pamoja na kujitangaza uwezo wao ili waweze kupata nafasi katika timu mbalimbali za kitaifa.

Aidha amewasisitiza waamuzi wa michezo kutenda haki kwakuwa matendo yao ni darasa la nidhamu na maadili kwa wanafunzi wao na kuwatahadharisha wanafunzi wasio tii kuwa hawatapata nafasi katika timu ya Mkoa.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Mageni Lutambi amewapongeza wakurugenzi wa halmashauri kwa kufanikisha upatikanaji na ushiriki wa timu za michezo za kila halmashauri.

Dkt. Lutambi ameishukuru pia kampuni ya Coca cola kwa udhamini wa UMISSETA kwa kutoa vifaa kwa shule 118 ambavyo ni tisheti 3,776, mipira ya miguu 118 na mipira ya basketball 118 pamoja na ahadi ya kuendelea kugawa vifaa katika shule 45 zilizobaki.

Ameongeza kwa kuwasihi wana michezo wote kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu, kwa kuzingatia sheria na kanuni za michezo ili kutengeneza timu ya ushindi ya mkoa.

Akisoma taarifa ya Michezo ya Umiseta Afisa Michezo wa Mkoa Henry Kapella amesema jumla ya wana michezo 576 wameshiriki katika michezo hiyo ambapo wataunda timu ya mkoa ya michezo ya bao, riadha, mpira wa miguu na mpira wa pete. 

Kapella ameongeza kuwa kauli mbiu ya michezo ya Umisseta kwa mwaka 2017 ni ‘Wekeza katika michezo kwa ustawi wa elimu na Viwanda’. 

Kwa upande wao wanafunzi walioshiriki mashindano ya umisseta wamesema michezo inawajenga kiafya na kiakili kwa kuwa wanafunzi wanaoshiriki katika michezo huwa na ufaulu mzuri wa masomo yao.

Wameongeza kuwa michezo inawaongezea nidhamu na kuwajenga kimaadili hivyo kufaulu inakuwa ni rahisi, aidha wamesema michezo ina faida nyingi ikiwemo kuwatengenezea ajira mara baada ya kumaliza masomo yao.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (aliyenyanua ubao) akipiga ubao wa kuashiria uzinduzi wa michezo ya UMISSETA mkoa wa Singida, mbele yake ni wanariadha wakianza mashindano.
 Wanamichezo kutoka Shule za Sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Itigi wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa, kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi na Kulia Kwake ni Afisa Elimu Mkoa wa Singida Florian Kimolo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia kabla ya kuzindua mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa wa Singida.
 Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA Mkoa wa Singida.
Afisa Michezo wa Mkoa wa Singida Henry Kapella akisoma taarifa ya michezo ya Umisseta wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ngazi ya Mkoa.

HIFADHI YA TAIFA MIKUMI MKOANI MOROGORO NI MBUGA ZA WANYAMA AMBAYO HUJIVUNIA IDADI KUBWA YA WAGEN

No comments:

 

Hifadhi ya Taifa Mikumi mkoani Morogoro ni moja ya mbuga za wanyama ambazo kwa sasa hujivunia idadi kubwa ya wageni na wanyama makundi tofauti wakiwemo simba pia ni hifadhi ambayo hufikika kwa urahisi na kuwafanya wageni kuona wanyama kwa haraka. 

Hifadhi imeshirikiana na vijiji katika kuunda ujirani mwema kupitia miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikiibuliwa na wananchi ili kuhakikisha maafisa wa wanyamapori wanashirikiana na wanavijiji kulinda mipaka ya hifadhi ya taifa mikumi dhidi ya ujangili. 

Mbuga ya wanyama Mikumi hupokea wageni wa aina mabalimbali wakimiwemo wenyeji wakazi kwa vingilio tofauti ukilinganisha na watalii wandani ambapo vingilio vyao ni shilling 5700 kwa mtu mzima.
 Muongozaji wa hifadhi ya taifa milima ya Udzungwa mkoani Morogoro Yuston Bonike akimuonyesha muandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Ashton Baraigwa mbegu ya mimea ambayo inaweza kuliwa na nyani kipindi cha ukosefu wa chakula na kumletea madhara na nyani huyo kugeuka kuwa kichaa.
Moja wa maporomoko ya maji kivutio ambacho kina patikana katika hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa mkoani Morogoro ambacho hufikiwa kirahisi kwa njia ya miguu na hupatikana ndani ya msitu huo.
Moja ya mnyama anayepatikana katika hifadhi hiyo anayejulikana kwa jina maarufu “digidigi” akiwa ndani ya Msitu huo 
Hali halisi ya mazingira ya hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa mkoani Morogoro ambapo ofisi zake hupatika hapo mbele
Mafundi wakiwa katika ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Lumango Wilayani Kilosa mkoani Morogoro mradi wa ujirani mwema unaotekelezwa na Hifadhi ya taifa mikumi kwa asilimia 70 huku wananchi wakichangia nguvu kazi kwa asilimia 30. Nia na madhumuni ya ushirikiano huo ni kulinda na kuhifadhi mipaka ya TANAPA pamoja na kutoa taarifa za ujangili.
Moja ya jengo la Zahanati ambalo limeanza kutumika katika Kijiji cha Ihombo kata ya Mikumi mkoani Morogoro ambayo hupokea wagonjwa wasiopungua 300 kwa mwezi mradi ambao ulitekelezwa na Hifadhi ya taifa Mikumi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema na ulinzi wa mipaka ya hifadhi hiyo.
Tembo nao ni miongoni mwa wanyama wanaopatikana kwa wingi katika hifadhi ya taifa Mikumi mkoani Morogoro ambao mara nyigi hupenda kutembea kwa makundi wakati wa kujitafutia malisho.
Kikundi cha utunzaji wa mazingira kinachotokana na mradi wa utalii wa kitamaduni wakiwa wameshikilia vikapu ambavyo vimetengenezwa na mifuniko ya chupa za maji ambayo wamekuwa wakiyaokota. Wa pili kutoka kulia ni katibu wa kikundi hicho Bw. Christandus Mdoe.
Wageni wa kitalii katika hifadhi ya taifa mikumi mkoani Morogoro wakijadiliana kitu nje ya ofisi ya mapokezi huku wakifurahia mazingira ya eneo hilo la wanyama wakionyesha jinsi walivyo na amani katika eneo hilo.
Silas Bakari fundi ujenzi wa nyumba za kitamaduni akionyesha matumizi ya vyumba katika maeneo ambayo yamejengwa na chupa ambazo huokotwa kandokando ya hifadhi ya taifa mikumi na maeneo mengine, jinsi ambavyo chupa hizo zitakavyoboreshwa na kuifanya nyumba kuwa kivutio ch a utalii wa kitamaduni kwa wageni.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JUNI MOSI,2017

No comments:


 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger