Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi imeweka mikakati mbalimbali ili kukabiliana na upungufu wa maziwa nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.Dk Charles Tizeba wakati akijibu swali la
Mbunge wa Wete Mhe.Mbarouk Salum Ali leo Bungeni MJini Dodoma katika
Kikao cha thelathini na sita cha bunge la 11.
Charles Tizeba
Charles Tizeba
“Nakubaliana na Mhe.Mbunge kuwa
Tanzania ina idadi kubwa ya mifugo lakini bado kuna upungufu wa
maziwa,ambapo takwimu za makadirio za mwaka 2016 zinaonyesha lita
bilioni 2.09 za maziwa zilizalishwa na unywaji wa maziwa kwa mtu kwa
mwaka ulifikia lita 47 ukilinganisha na lita 200 zinazopendekezwa na
Shirika la chakula Duniani(FAO)”,Alisema Mhe.Tizeba
Aidha kati ya Ngombe milioni 28.4,
Ngombe rasmi wa maziwa ni 782,995 tu sawa na asilimia 3 ya Ng’ombe
wote.Aidha kati ya mbuzi milioni 16.7 ni mbuzi rasmi takribani 50,000
ndio wa maziwa ambao ni asilimia 0.3 ya mbuzi wote.
Amezitaja jitihada ambazo Serikali
imechukua ili kukabiliana na upungufu wa maziwa nchini ni pamoja na
kumarisha mashamba ya kuzalisha mifugo ya Serikali (LMU’s) ili kuongeza
idadi ya Ng’ombe wenye uwezo wa kuzalisha maziwa kwa wingi.
Aidha Serikali imeanzisha vituo
vya uhimilishaji katika kanda 6 hapa nchini ambazo ni kanda ya
Ziwa(Mwanza),kanda ya Magharibi(katavi),Kanda ya kati(Dodoma),Kanda ya
Mashariki(Kibaha),Kanda ya Kusini(Lindi) na Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini(Mbeya) kwa lengo la kutoa huduma ya uhilimishaji wa Ng’ombe wa
Maziwa walioko kwenye maeneo hayo pamoja na Ng’ombe wa Asili ili
kuzalisha idadi kubwa ya Ng’ombe wa Maziwa.
Amehimiza kuwa Jitihada hizi
zitawezesha idadi ya Ng’ombe wa Maziwa kufikia milioni 2.9 ifikapo mwaka
2021/22 ambao pamoja na ng’ombe wa asili wataweza kuzalisha lita
bilioni 3.8 za maziwa.
“Serikali inaendelea kuhamasisha
sekta binafsi na wadau wengine wa maendeleo kuwekeza katika uzalishaji
wa mitamba ya maziwa na mashamba ya ng’ombe wa maziwa kwa lengo la
kuongeza uzalishaji wa maziwa hapa nchini”,Aliongeza Mhe.Tizeba
SHARE
No comments:
Post a Comment