Taarifa kwa vyombo vya
habari
MEI
21, 2017. Dawa maarufu ya meno ya Whitedent
imepata tuzo ya kimataifa ya ubora
inayojulikana kama SuperBrand kutokana na utafiti uliofanywa kwenye masoko nchini na kampuni ya kimataifa ya utafiti wa ubora wa
bidhaa ya nchini Uingereza inayojulikana
kama The Centre for Brand Analysis ambapo imeshikia nafasi ya kwanza nchini
Tanzania kwa mwaka 2017.
Katika utafiti huo uliofanyika katika masoko kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Arusha , Mwanza na
kuwahusisha wananchi mbalimbali zaidi ya 1,000 watumiaji wa bidhaa na huduma
pia sabuni maarufu ya unga ya Foma Gold nayo imebainishwa kuwa ni bidhaa bora
hapa nchini nayo imetunukiwa tuzo ya
SuperBrand ikiwa inashikilia nafasi ya pili.
Akiongea kuhusu matokeo ya chapa bora zinazokubalika wa kiasi kikubwa nchini,Afisa Mtendaji wa
taasisi ya The Centre for Brand Analysis,Stephen Cheliotis,alisema kuwa
inafurahisha kuona chapa nyingi za Tanzania zinaendelea kushikilia rekodi ya
ubora na kuendelea kupata tuzo SuperBrand mwaka hadi mwaka wakati huohuo
zikijitokeza chapa mpya ambazo zinafanya vizuri kwenye masoko.
"Mwaka huu chapa nyingi zimeweza kuendelea kushikiria
rekodi ya kuingia kwenye chapa bora 20
zinazoongozwa kwenye masoko na mwaka huu chapa za bidhaa kwenye kundi la usafi na afya za Whitedent na Foma Gold
zimefanya vizuri na katika utafiti wetu tumegundua kuwa zinakubaliwa na wengi
kwenye masoko kutokana na kuwa na viwango vya juu vya ubora," alisema Stephen
Cheliotis.
Amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ulizingatia maoni ya
watalaam wazoefu wa masoko na walengwa wa huduma za bidhaa ukihusisha pia
makampuni ya hapa hapa nchini yanayotumia nembo cha chapa za biashara za
kimataifa kama vile TOYOTA na Pepsi ambapo chapa 10 zimeendelea kuingia kwenye
chapa 20 bora na utafiti huo ulifanyika
katika mgawanyo wa makundi ya taasisi za
fedha,vyakula na vinywaji,magari na utoaji wa huduma kwa jamii.
Chapa za Tanzania 20 ambazo zimepata tuzo ya Super Brand
2017 ni White Dent ambayo imekuwa kinara ikifuatiwa na Foma Gold.Nyingine
zimetajwa kuwa ni Maji ya kunywa ya Kilimanjaro,Panadol,ITV,Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam.
Nyingine ni Mlimani City,Chai Bora,Benki ya NMB,Kampuni ya Vodacom,Benki
ya CRDB,Konyagi,kituo cha redio cha Clouds FM,gazeti la Mwananchi,Maji ya Uhai
ya Azam,Toyota,Huduma ya M-Pesa ya Vodacom,Hedex,Pepsi na maduka ya Nakumatt.
SHARE
No comments:
Post a Comment