Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akizungumza na wanahabari
wakati wa kutoa zawadi kwa watoto Yatima wa Kituo cha Mtoto Wetu
Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akiwa amekaa na watoto wa kituo hicho.
Mratibu wa Miradi wa Kampuni hiyo, Gasparino Haule akiongoza kucheza katika hafla hiyo.
Ofisa Rasilimali Watu wa Kampuni hiyo, Grace Zikwaze, akizungumza na watoto hao.
Keki maalumu ya hafla hiyo ikikatwa kwa pamoja. Kushoto ni Makamu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Theobald Truphone na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo. Wengine ni maofisa wa Kampuni ya Trumark.
Zawadi zikitolewa.
Mwanafunzi Shafii Hassan wa kituo hicho akizungumza
kwenye hafla hiyo.
Mwanafunzi Wanswekula Zacharia akizungumza na wanahabari kuhusu changamoto walizonazo.
Nguo zikiandaliwa tayari kukabidhiwa watoto hao.
Keki maalumu kwa ajili hayo iliyotolewa na Kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akiwalisha keki watoto hao.
Watoto wakiserebuka.
Ofisa Utawala wa Kampuni hiyo, Azavery Phares akimkabidhi keki hiyo maalumu, mtoto Godwin Steven.
Picha ya pamoja kabla ya kuicharanga keki hiyo tayari kwa kuila.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akiwa na watoto wake kwenye hafla hiyo.
……………………………………………………………………..
……………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
JAMII imetakiwa kujenga moyo wa kusaidia watu waliopo katika makundi yenye uhitaji ili nao wajisikie kama watu wengine waliopo katika familia.
Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark inayojishughulisha na uwezeshaji jamii, Agnes Mgongo wakati kampuni hiyo ilipokuwa ikitoa zawadi ya Sikukuu ya Eid El-Fitr katika Kituo cha watoto Yatima cha Mtoto Wetu Tanzania kilichopo Kimara Suca jijini Dar es Salaam leo hii.
“Ni vizuri jamii ikajenga tabia ya kuwakumbuka watoto na watu wengine waliopo katika makundi maalumu kwa kuwafariji badala ya kuiachia serikali ambayo ina mambo mengi ya kufanya” alisema Mgongo.
Alisema kampuni yake iliguswa na changamoto walizonazo watoto waishio katika kituo hicho ikaona ni vizuri katika kipindi hiki cha sikukuu ya Eid El-Fitr wakajumuike nao kwa kula na kucheza pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali.
Mgongo alitaja zawadi walizotoa kupitia wadau wengine marafiki wa taasisi hiyo kuwa ni nguo, vinywaji na chakula ambacho kilipikwa katika kituo hicho.
Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo watoto waliopo katika makundi yenye uhitaji, Wanswekula Zacharia alisema ni pamoja na vitabu, karo, sare za shule na mahitaji mengine.
Alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo mwanafunzi anapaswa kujua wajibu wake akiwa shuleni ni kusoma na si vinginevyo.
Alisema kupokea misaada ni jambo moja lakini hata mtu kufika tu kituoni hapo na kuwajulia hali bila ya kuwa na kitu chochote ni jambo la heri kwani wanachohitaji zaidi ni kujumuika na jamii na kupata faraja.
Mwanafunzi wa kidato cha sita, Shafii Hassan ambaye analelewa katika kituo hicho tangu akiwa mdogo anasema misaada wanayoipata imekuwa ikiwafanya wapate faraja ukizingatia ukubwa wa changamoto walizonazo.
Makamu Mkurugenzi wa Kituo hicho,Theobald Tryphone aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kueleza changamoto kubwa walizonazo ni ada za wanafunzi, chakula, ulipaji wa umeme na kuwa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) wameweka alama za x katika majengo yao waondoke lakini suala hilo linashughulikiwa na Manispaa ya Ubungo kuona jinsi itakavyowasaidia kuwasaidia kupata eneo jingine kwa ajili ya
kujenga kituo hicho.
Mtoto analelewa katika kituo hicho, Godwin Steven alitoa shukurani kwa kampuni hiyo kwa niaba ya wenzake kwa msaada huo.
SHARE
No comments:
Post a Comment