TRA

TRA

Tuesday, June 13, 2017

Moto mkubwa wateketeza jengo refu la makazi London

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Jengo moja la ghorofa limeshika moto katika barabara ya Latimer, magharibi mwa jiji la London, watu walio shuhudia tukio hilo wanasema, moto huo umeleta mshituko mkubwa hali iliyosababisha baadhi ya watu kushindwa kutoka katika makazi yao.

Taarifa zinadai kuwa baadhi ya watu bado wamekwama ndani ya jengo hilo linalo waka moto.

Moto huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza mwendo wa saa 01:16, saa za Uingereza na karibu wazima 200 wanapambana nao.
Hadi sasa moto huo unaendelea kuunguza jengo hilo vikosi vya uokoaji na zima moto takriban 200 vikiendelea na kazi hiyo.

 Idara ya wazima moto jijini London imetuma malori 40 ya kuzima moto huo

Idara ya wazima moto jijini London imetuma malori 40 ya kuzima moto huo
Polisi wanamesema kuwa hadi sasa imebainika kuwa ni watu wawili tu ambao wameathirika na moshi wa moto huo na wanapata matibabu huku idadi ya waliokwama ndani ya jengo hilo ikiwa haijulikani.

Mwandishi wa BBC Andy Moore aliyepo katika eneo la tukio kwa sasa anasema jengo hilo lina hatarini kuanguka wakati wowote.

 CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger