Baadhi
ya wapagazi zaidi ya 300 wakijiandaa kwa ajili ya safari ya kupanda
Mlima Kilimanjaro katika lango la lemosho kusindikiza ugeni wa kund la
wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa kutoka mataifa
mbalimbali nchini .
Wachezaji
wa timu za taifa kutoka mataifa mbalimbali nchini ,wakishuka katika
gari mara baada ya kuwasili katika lango la Lemosho kwa ajili ya kuanza
safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuweka historia ya
kucheza mchezo a kirafiki eneo la Kreta katika kilele cha Uhuru.
Mchezaji
wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ,Twiga Stras ambaye kwa sasa
anakipiga timu ya IFA Academy ya nchini Dubai,Rajvi Ladha akifurahia
jambo na Ofisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey
Tengeneza.
Mchezaji
wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania ,Twiga Stars ,Rajvi Ladha
akiandika jambo muda mfupi baada ya kuzungumza na wanahabari juu ya
mchezo huo ,
Wachezaji
wa timu za Volcano fc na Gracier fc wakikamilisha taratibu kabla ya
kuanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya mchezo wa
kirafiki utakao pigwa June 26 mwaka huu katika kilele cha Uhuru.
Afisa Uhusiano Mkuu wa TTB ,Geofrey Tengeneza akipata taswira ya pamoja na wachezaji hao.
Afisa
Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini,TTB Geofrey Tengeneza akieleza
jambo kwa wachezaji hao muda mfupi kabla ya kuanza safafri ya kupanda
Mlima Kilimanjaro.
Mwakilishi
wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Willy Lyimo akizungumza na wachezaji hao
kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya wachezaji wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.
SHARE
No comments:
Post a Comment