TRA

TRA

Monday, June 19, 2017

Rais wa FIFA aridhishwa na Kombe la Mabara

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Michuano ya Kombe la Mabara huwashirikisha mabingwa wa mabara, mabingwa wa Dunia pamoja na taifa litakaloandaa Kombe la Dunia lijalo, na hutumiwa kama kionjo au matayarisho ya Kombe la Dunia katika mwaka unaofuata
Lakini kabla ya kuanza dimba hilo, kulikuwa na tetesi za hapa na pale kuhusiana na umuhimu wa michuano hiyo, na hata wengine walidai kuwa hii huenda ikawa awamu ya mwisho ya dimba hilo la mabara kabla ya kufutiliwa mbali. 

Lakini Rais wa FIFA Gianni Infantino ameeleeza kuridhishwa kwake na namna michuano hiyo ilianza Urusi mwishoni mwa wiki ijapokuwa hajazungumzia kuhusu mustakabali wake.

Akizungumza kabla ya mechi ya Chile na Cameroon, Infantino alisema dimba hilo limeanza kwa kasi inayostahili na kuwa mashabiki waliburudishwa na mchuano wa ufunguzi ambao wenyeji Urusi waliwalaza New Zealand mabao mawili kwa moja. 

Rais huyo wa FIFA anasema ni wakati wa kuzingatia kandanda lenyewe na sio kuzungumzia mustakabali wa dimba hilo
Mrundiko wa mechi una maana baadhi ya makocha wa kimataifa wanaamini kuwa kinyang'anyiro hiki kinachosha. 

Idadi ya mashabiki wanaofika viwanjani na kutizama kwenye televisheni ni ndogo kuliko michuano ya kiwango cha juu ndio maana hata haishangazi kuwaona mabingwa wa dunia Ujerumani wakipeleka timu ya pili isiyokuwa na wachezaji wengi vigogo

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger