TRA

TRA

Monday, June 19, 2017

Ujerumani yaitambia Australia kombe la mabara

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
 
Timu ya taifa ya Ujerumani imeichapa timu ya Australia kwa mabao 3-2 katika mchezo wa kundi wa kombe la mabara michuano inayofanyika nchini Urusi.

Iliwachukua dakika tano tu kwa Ujerumani kuandika bao la kwanza kupitaia mshambuliaji wa ke Lars Stindl, Australia wakasawazisha goli hilo katika dakika ya 41 kwa goli la Tom Rogic.

 Wachezaji wa Ujerumani na Australia wakipongezana baada ya mchezo kumalizika
 
Mshambuliaji matata wa Ujerumani Julian Draxler akaongeza goli la pili kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 45.

Dakika ya 48 Ujerumani waliongeza bao la tatu kupitia kwa kiungo Leon Goretzka, goli la pili la Austaria lilifungwa na mshambuliaji Tomi Juric anayekipiga katika klabu ya FC Luzern.

CHANZO:BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger