Rais wa Marekani
Donald Trump anatarajiwa kutangaza mabadiliko ya sera kuihusu Cuba na
kukaza zaidi kamba ya vikwazo vya usafiri ambavyo vilikuwa vimelegezwa
na rais Obama.
Donald Trump bado anaonekana kuwa na azma ya kubatili sera zote za mtangulizi wake Barack Obama.
- Donald Trump asema Fidel Castro alikuwa ‘dikteta katili’
- Trump atishia kufuta sera za Obama kuhusu Cuba
- Trump na Obama watofautiana kuhusu Fidel Castro
Rais Obama alikuwa amelegeza vikwazo hivyo katika hatua ya kuimarisha uhusiano kati ya Washington na Havana.
Hata hivyo wamarekani bado wataruhusiwa kuzuru kisiwa hicho cha kikomunisti lakini kupitia makundi yaliyotambuliwa.
Biashara kati ya marekani na jeshi la Cuba katika sekta ya utalii na kiviwanda pia itatiwa kikomo na bwana Trump.
Makundi kadhaa ya kutetea haki yameitaka marekani kuendelea kuzungumza na Cuba yakisema kuwa miongo kadhaa ya kuitenga Cuba haijaimarisha haki za kibinadamu nchini humo.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment