Mpango
mpya unaohamasishwa na wadau wa sekta ya kilimo hatimaye utawapa
wakulima wadogo nchini kote fursa ya kupata masoko ya uhakika na
endelevu kwa kuepuka madalali wa mazao yao.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Farm
Africa jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkazi wa Tanzania wa Farm
Africa, Steve Ball alisema kuwa warsha hiyo ililenga kuwafudisha
wakulima namna bora kuingia kwenye mfumo rasmi wa biashara ya nafaka.
Alisema
kuwa jukwaa hilo la wadau kwenye sekta hiyo linaunganisha biashara
nzima ya nafaka kutoka kwenye shamba hadi sokoni na inashirikisha
mkusanyiko wa programu zinazoruhusu watumiaji kusimamia hesabu, mazao ya
biashara, soko endelevu na kupata mikopo kutoa kwenye taasisi za fedha.
"Tuko
hapa kuzungumza juu ya njia bora ya kuwasaidia wakulima wadogo ili
kuepuka madalali wakati wa kutafuta masoko ya mazao yao na ili waweze
kupata kwa bei bora zaidi baada ya kupata taarifa sahihi na kwa wakati
muafaka juu ya mwenendo wa soko,” alisema.
Aliongeza
pia kwamba wadau katika sekta hiyo wana matumaini kwamba wakulima
watakusanya nguvu kwa pamoja na kutengeneza maghala yao ya kuhifadhi
mazao yao na kuuza kwa pamoja ili kupata bei nzri zaidi.
Alibainisha
kuwa kwa njia ya G-Soko, wakulima wanaweza kuunganisha mavuno yao
kupitia ghala lao na kuthibitishwa na kupata huduma za kifedha kwa
kutumia nafaka zao kama dhamana. Jukwaa pia hutoa programu ya malipo ya
huduma na ukusanyaji wa data wa wakulima.
Alifafanua
kamba wadau wanajua kwamba zuio la serikali kuuza chakula ni kudhibiti
hali ya uchumi wa nchini na vile vile kuzuia kununua unga, mchele kutoka
nje baada ya wakulima kuuza mahindi na mtama lakini aliongeza ni muhimu
kwa serikali kuwajengea wakulima uwezo ili kuanzisha viwanda vya
kusindika vyakula hapa hapa nchini.
Kwa
upande wake, Mshauri wa Sera kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi,
Revelian Ngaiza alisema kuwa serikali inatafuta njia bora ya kupunguza
gharama za shughuli za kilimo kwa mkulima mdogo kwa kuboresha mfumo wa
miundombinu, usafiri na usambazaji.
"Kuboresha
upatikanaji wa habari kwa wakulima wadogo juu ya bei ya soko na
mahitaji ya walaji na kuwezesha ushirikiano na sekta binafsi na serikali
katika kumuinua mkulima mdogo vijijini,’ alisema.
Alisema
serikali ina nia ya kuanzisha mikakati na sera mbalimbali za
kubadilisha kilimo ili kuendeleza utendaji bora na uboreshaji
ulioimarishwa na ukuaji wa uchumi.
"Katika
Tanzania peke yake, karibu asilimia 40 nafaka hupotea kutokana na
uhifadhi duni na mabadiliko ya hali ya hewa kila mwaka, kwa gharama ya
dola za Kimarekani milioni 332 na kuacha wakulima wa nafaka kwenye
hasara kubwa," alisisitiza
Shirika
lisilo kuwa la kiserikali la Mipango ya Maendeleo Mjini na Vijijini
(RUDI), Afisa Mtendaji Mkuu wake, Lameck Kikoka ana matumaini kuwa
kuingilia kati kwa wadau hao wa kilimo nchini na mashirika ya kimataifa
ya kilimo kutasaidia wakulima zaidi ya 30,000 nchini Tanzania pekee
kupata masoko zaidi, hivyo kupambana na umaskini na kuboresha ustawi wa
wakulima.
Alisema
kuwa zamani changamoto za wakulima zilikuwa kubwa gharama kubwa za
pembejeo kama vile mbegu zilizoboreshwa na mbolea na wengi walikuwa
hawana mahali pa kuhifadhi mazao yao wakati wanasubiri bei bora kwenye
soko.
"Lakini
kuingilia kati kwa serikali na kuanzisha mfumo wa stakabadhi ghalani
kutaendelea kuwahahikishia wakulima bei bora na usalama wa mazao yao na
soko endelevu kwa mazao yao wakati na kuongeza uwezo wao wa kuhifadhi
kwa kuendelea kujenga maghala yao wenyewe yatakayo thibitishwa na
serikali,” alifafanua.
"Ili
kusaidia wakulima kufaidika na fursa hizi, Farm Africa na washirika wa
ushirika (RUDI) sasa wanataka kusaidia wadogo wa Tanzania na Uganda
kushika mchele, mazao na maharage ya ziada."
"Tunapaswa
kulima na kuvuna zaidi baada y kupata uelewa wa mfumo rasmi wa
biashara ya nafaka na uelewa wa kupata soko la uhakika bila madalali ,"
alisema Emerita Singaile. Mwenyekiti wa Umoja wa wakulima wa Makalali
kutoka mkoani Iringa
Mkurugenzi
Mkazi wa Farm Africa, Steve Ball akizungumza kuhusu umuhimu wa wakulima
kupata taarifa za uhakika kuhusu mwenendo wa masoko, wakati wa warsha
ya wadau wa mazao ya nafaka iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment