WAKATI lile sakata Linalomuhusu kijana Said Mrisho anayedaiwa kutobolewa macho na mtu aitwaye, Salum Njwete ‘Scorpion’ kumtelekeza mkewe, Stara Sudi ‘Mama D’ na watoto wanne, likiwa bado bichi, jipya jingine limeibuka ambapo wawili hao wameanza kugawana mali.
Tukio
hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Maji-Chumvi,
Tabata-Kimanga jijini Dar, zikiwa zimekatika siku chache tangu Stara
apangishiwe nyumba na Said kisha jamaa huyo kwenda kuishi na mwanamke
mwingine mwenye asili ya Kiarabu.
Akizungumza na Wikienda, Stara alisema kuwa amefi kia uamuzi huo wa kuchukua kilicho chake baada ya kutelekezwa kwenye nyumba hiyo.
“Amenitelekeza,
nitakaa vipi hapa… nimeamua kuchukua vitu na kupeleka nyumbani kwetu.
Nimekaa hapa kwa siku nne tu, nimekuja kuchukua malipo yangu ya miezi
mitatu.
Ujue
mwanzoni tulikubaliana na Said na akamuomba mwenye nyumba kuwa atakuwa
akilipia kodi miezi mitatu-mitatu, lakini mama yangu akakataa, akasema
muongo huyo, atakukimbia na kwamba kwa nini kwangu alipie miezi mitatu
na kule (kwa mke mwingine) alipie miezi tisa? Said akadhani nitajua
amesafi ri ili awe anakuja kwa siri kuchukua vitu kidogokidogo,” alisema Stara.
Kwa upande wake, Said alisema kuwa, alikubaliana na hatua aliyoichukua Stara ya kuchukua vitu vyote ikiwemo friji, makochi na vingine vingi, jambo lililofanywa mbele ya mashahidi akiwemo mwenye nyumba.
“Nilikuwa
ninatoa pesa vizuri, ilifi ka kipindi nikamwambia akatafute nyumba ya
laki moja, akaenda kutafuta ya shilingi laki moja na nusu, nikalipia
kwani niliomba kulipia miezi mitatumitatu.
Nashangaa
kuambiwa kuwa nimetelekeza familia, hivyo ni visingizio ambavyo
mwenzangu amewahi kwenda kwenye media na kuongea bila kusikiliza upande wangu,” alisema Said na kuongeza:
“Nilipigiwa
simu na mwenye nyumba kuwa amepaki kila kitu kwenye gari, anahama na
ameshapeleka barua Ustawi wa Jamii (Ilala) kuwa ninahitajika siku ya
Jumatatu (leo) na kwamba kiasi cha kodi kilichokuwa kimelipwa (laki nne
na nusu) arudishiwe kwani ndiyo kwanza amekaa miezi minne.
Nilifi ka na kufanya makabidhiano mbele ya mwenye nyumba.”
SHARE
No comments:
Post a Comment