TRA

TRA

Saturday, July 29, 2017

CHEZEA DIAMOND WEWE. AMPELEKA ZARI KUPUMZIKA MOMBASA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 

Ni siku chache zimepita toka Zari ambae ni Mama watoto wa Mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond Platnumz afiwe na Mama yake mzazi nyumbani kwao Uganda, msiba ambao umetokea mwezi mmoja baada ya Zari kufiwa na Baba watoto wake aitwae Ivan.
Mitandaoni kumekua na maneno mengi ya mashabiki wakisema Zari hajaonekana kama ana huzuni kwenye misiba na kwamba hajawa na majonzi kama kweli kafiwa na Mama yake.
Wakati hayo yakisemwa, Diamond amemchukua Zari na kumpeleka Mombasa Kenya kwa mapumziko na kumliwaza baada ya kupata misiba hiyo ambapo D aliwatolea makavu wanaojifanya wana uchungu wa misiba ya watu.
Diamond alisema kuna watu wanajifanya wanajua sana uchungu wa msiba ya watu “Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo anatakiwa apelekwe sehemu tulivu apetiwepetiwe adekezwe apate faraja! sasa kama nyie hamna mabwana wa kuwafanyia hayo msijifanye ni tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie”
“Eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia.. pambaneni na mahusiano yenu, nina siku 5 za kumpetipeti leo ndio kwanza ya kwanza”

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger