Mahakama
ya Delhi, India imemhukumu raia wa Tanzania ambaye alikamatwa na dawa za
kulevya ikisema imefanya hivyo si tu kwa sababu ya kujihusisha kwenye
biashara hiyo bali pia ili iwe funzo kwake.Katika taarifa iliyochapishwa
na DNA (Daily News & Analysis) India, Ramadhan Ismail mwenye umri
wa miaka 32 amekiri kosa akisema sababu ya kujiingiza kwenye biashara
hiyo ni umasikini na majukumu ya katika familia.
Jaji
maalum aliyeshughulikia kesi hiyo Sudesh Kumar
alisema: ”Sababu kuu ya kumfunga mtuhumiwa siyo kufanya kosa
pekee. Mahakama, wakati zinamuhukumu mtuhumiwa, lazima zijaribu, ndani
ya sheria, kutoa nafasi kwa mtuhumiwa kujirekebisha na kumuongoza katika
maisha ya kawaida, awe mtumishi wa jamii.” – Jaji Sudesh Kumar.
Adhabu
hiyo imetolewa na Mahakama baada ya Ismail kupatikana na hatia ya
kusafirisha 25kg za ephedrine ambapo alikamatwa na John Gugu, July 10,
2015, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Indira Gandhi (IGIA).
Mtetezi
wa Ismail, Anup Gupta alisema mtuhumiwa huyo alijiingiza kwenye kesi
hiyo kutokana na umasikini akisema pia ni mgonjwa na amepoteza 38kg
tangu alipokamatwa.
Anup
Gupta aliieleza Mahakama kuwa:Familia yake inajumuisha mama
yake ( 56), bibi yake ( 81), kaka zake watatu na dada yake. Hakuna mtu
atakayewaangalia. Baba yake ameitelekeza familia muda mrefu," alidai Gupta.
Mahakama
imemhukumu kifungo cha muda alioutumikia na kulipa faini ya Rs 50,000,
na akishindwa kufanya hivyo atatumikia kifungo rahisi cha mwezi mmoja.
SHARE
No comments:
Post a Comment