TRA

TRA

Saturday, July 15, 2017

DK. JANE GOODALL ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA YA KUTAMBUA MCHANGO WA UTAFITI WAKE WA MIAKA 60 YA MAISHA YA SOKWE HIFADHI YA GOMBE TANZANIA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


01
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) akimkabidhi  Dk. Jane Goodall tuzo maalumu ya heshima kwa kutambua mchango wake wa utafiti wa miaka 60 wa maisha ya Sokwe katika hifadhi ya Gombe iliyoko mkoani Kigoma   pamoja na uhifadhi wa wanyama wengine kwenye hifadhi hiyo,   katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Tuzo hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA).
1
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANAPA Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara akisalimiana na Dk. Jane Goodall wakati alipowasili kwa ajili ya kupokea tuzo yake leo.
02
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) akimkabidhi  Dk. Jane Goodall tuzo maalumu ya Heshima kwa kutambua mchango wake wa utafiti wa miaka 60 wa maisha ya Sokwe katika hifadhi ya Gomb.
2
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANAPA Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara akizungumza na Dk. Jane Goodall kabla ya kupokea tuzo hiyo.
03
Dk. Jane Goodall akivishwa zawadi ya vitenge na  Getrude Mongela wakati wa kupokea tuzo maalumu ya heshima.
3
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Balozi Sara Cook kabla ya kukabidi tuzo kwa Mtafiti wa Sokwe Dk. Jane Goodall, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Dk. Jane Goodall Foundation, James Lembeli.
04
Dk. Jane Goodall akipokea pia zawadi ya picha ya sokwe Sokwe kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe,  kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Dk. Jane Goodall Fuondation Bw. James Lembeli na Mama Getrude Mongella na kutoka kushoto ni Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania  Balozi Sara Cook na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANAPA Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara.
4
 Dk Jane akitoa maelezo kuhusu maisha ya Sokwe kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Dk Jane Goodall Foundation Bw. James Lembeli.
6
Dk. Jane Goodall akipatiwa pia zawadi ya kinyago cha Sokwe kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe,  kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Dk. Jane Goodall Fuondation Bw. James Lembeli na Mama Getrude Mongella na kutoka kushoto ni Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania  Balozi Sara Cook na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANAPA Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara.
7
Dk. Jane Goodall akionyesha cheti maalum baada ya kupokea tuo kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe  katika picha kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Dk. Jane Goodall Fuondation Bw. James Lembeli na Mama Getrude Mongella na kutoka kushoto ni Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania  Balozi Sara Cook na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANAPA Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara.
8
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe  akizungumza katika hafla hiyo.
9
 Wasanii wa Tanapa wakitumbuiza kwa wimbo 
10
Balozi Sara Cook akizungumza katika hafla hiyo.
11
Mkurugenzi wa TANAPA Dk. Allan Kijazi akizungmza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Chuo cha Utalii cha Taifa.
12
Baadhi ya Mabalozi waliohudhuria katika hafla hiyo.
14 ……………………………………………………..
Habari na Richard Mwaikenda Jane ambaye ni raia wa Uingereza alianza utafiti katika Hifadhi ya Gombe mnamo miaka ya 60 akiwa na umri wa miaka 26. Katika utafiti wake amegundua mambo mengi ikiwemo jinsi Sokwe wanavyojitambua, kuwa na hisia na jinsi wanavyoishi kwa ushirikiano kama walivyo binadamu.
Akizungumza katika hafla hiyo jane anasema wakati anaanza kufanya utafiti ilikuwa vigumu Sokwe hao kumkaribia kwani walikuwa wanamuogopa na ilikuwa ni mara ya kwanza kwao kumuona mtu mweupe, lakini alifanya jitihada hadi wakamzoea na kuanza kumsogelea na kumuona mtu wao wa karibu.
Anasema alitumia mbinu mbalimbali kama vile kuwapatia ndizi na vyakula vingine hadi wakamzoea.

Wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Utalii katikati ya jiji la Dar es Salaam, viongozi na wageni waalikwa walipata wasaa wa kuangalia picha mbalimbali za matukio ya sokwe wakiwa na Jane Goodall.
Katika utafiti wake amefanikiwa kuanzisha chuo na kutunga vitabu pamoja na video zinazoelezea maisha yake na Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma.

Katika hafla hiyo walihudhuria Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali George Waitara, Mwanasiasa Mkongwe, Getrude Mongela, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Goodall, Lembeli, Balozi wa Uingereza nchini, mabalozi mbalimbali pamoja na waalikwa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger