Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Maneromongo katika mkutano wa kuhamasisha maendeleo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akishuhudia
upangaji wa mawe katika moja ya majengo yanayojengwa wilayani Kisarawe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitoa
maelekezo kwa Afisa Elimu msingi wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Bane
alipotembelea ukarabati wa Shule ya msingi Kwala
Ujenzi wa madarasa na mabweni unaoendelea katika shule ya
sekondari Maneromango
Wananchi wa kata ya Maneromango wakiwa katika mkutano wa pamoja
na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ameagiza
maafisa elimu nchini kuboresha mazingira ya shule za msingi na sekondari katika
halmashauri zao wanazoziongoza ili ziwe na mandhari ya kuvutia.
Jafo ametoa maagizo hayo alipokuwa akitembelea ujenzi wa
madarasa, vyoo, na mabweni katika wilaya ya Kisarawe.
Katika ziara yake, Jafo amefurahishwa sana na ujenzi unavyo
endelea wilayani humo kwa ulazaji wa matofali katika majengo yote kutokana na
ujengaji wa aina hiyo unayafanya majengo kuwa na ubora mkubwa.
Naibu Waziri Jafo ametaka mazingira ya shule zote nchini yawe
safi kwa kupanga mawe pembeni na barabara, kupanda majani, maua na miti ili
shule ziwe kivutio kwa watoto.
Jafo alitembelea na kukagua ujenzi katika Shule ya msingi Kwala
ambayo kuna ujenzi wa vyumba vya Madarasa matatu, matundu ya vyoo kumi na mbili
pamoja na ujenzi wa ofisi ya walimu.
Pia alitembelea ujenzi wa mabweni mawili, vyoo matundu kumi na
sita, madarasa matatu, na ujenzi maktaba katika shule ya sekondari Maneromango
ambayo inatarajiwa kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano.
SHARE














No comments:
Post a Comment