KAMPUNI ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa
mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya
CIPESA ya nchini Uganda imefanya kongamano la kuwakutanisha wadau wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania ikiwa ni
kujadili masuala mbalimbali ya huduma za habari na mawasiliano pamoja na
kuangalia namna ya kulinda usiri wa taarifa za wateja wanaotumia huduma
hizo. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello alisema kongamano hilo limekuwa
na matokeo chana baada ya wadau kujadili masuala mbalimbali ya ICT lengo
likiwa kuboresha zaidi huduma hiyo na usalama kwa watumiaji. Alisema
wadau wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa
sheria za kusimamia huduma nzima ya ICT lakini wakashauri ufanywe kwa
kutoa fursa za maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa
watumiaji wa huduma za ICT. Alisema wadau wengi katika kongamano hilo walihoji kitendo cha Sheria
ya Makosa ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) kuanza kutumika bila
ya uwepo wa kanuni jambo ambalo limewapa ugumu hata watekelezaji na
wasimamizi wa sheria husika. Mkurugenzi huyo aliongeza Jamii Media
itaendelea kusaidia kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa huduma za
mawasiliano wakiwemo bloggers ili kuona wanakuwa na uelewa na matumizi
mazuri ya mitandao yao kupunguza mkanganyiko kwa wanufaika.
No comments:
Post a Comment