Aidha, Mnyika amemuomba Spika kutangaza wateule ambao wametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi Julai 27, 2017 kuwa hawataapishwa mpaka mashauri yao yaliyopo Mahakamani yamalizike.
Hatua ya John Mnyika imekuja siku chache baada ya Spika kuridhia kufutiwa uanachama Wabunge wanane wa CUF baada ya kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wake Prof. Lipumba kisha kutangaza nafasi zao kuwa wazi na kumuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya taratibu zilizostahili ambapo alitangaza majina ya Wabunge wengine wanane kuziba nafasi zao.
SHARE
No comments:
Post a Comment