Katibu wa Halmashauri kuu Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Humphrey Polepole akizungumza
na wanachama viongozi wa mashina pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa
wa Morogoro wakati alipofanya ziara ya kikazi katika kata ya Kidatu
wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.
Viongozi mbalimbali wa mashina na
matawi kata ya Kidatu wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro wakimsikiliza
Katibu wa Halmashauri kuu Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Ndugu Humphrey Polepole.
…………………………………………………………………………
Wajumbe wa kamati ya siasa ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya kidatu wamejiuzulu nafasi zao za
uongozi kwa pamoja na kuomba radhi wanachama kwa makosa ya kushindwa
kutoa uongozi madhubuti.
Akiwa katika ziara ya kichama
mkoa wa Morogoro Wilaya ya Kilombero kata ya Kidatu, tarehe 28 Julai
2017, Katibu wa Halmashauri kuu Itikadi na Uenezi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Ndugu Humphrey Polepole alifanya kikao cha ndani,
alipata fursa ya kuzungumza, kusikiliza na kutatua changamoto
mbalimbali za wanachama.
Katika kikao hicho kilichohusisha
Wanachama, Viongozi wa Mashina, Halmashauri kuu za Matawi na Kamati ya
siasa ya kata ya Kidatu, Ndugu Polepole aliambatana na viongozi
mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo Katibu wa Chama Cha
Mapinduz(CCM) Mkoa wa Morogoro, Katibu wa Chama wilaya, Mkuu wa mkoa wa
morogoro na mkuu wa wilaya ya kilombero.
Wakati wa kikao hicho
kilichoongozwa na Ndugu Polepole baada ya malalamiko na shutuma nyingi
kutoka kwa wanachama dhidi ya viongozi wa CCM kata ya kidatu ikiwemo
kushindwa kusimamia uchaguzi wa matawi, kushindwa kusimamia rasilimali
za chama, usaliti wakati na baada ya uchaguzi mkuu hali iliyopelekea
CCM kupoteza kata ya kidatu viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa
CCM kata ya kidatu Ndugu Mangungu Alex waliomba kujiuzulu nafasi zao
zote za uongozi ndani ya chama, kuomba radhi wanachama wa CCM na
kuahidi kubaki kuwa wanachama waaminifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akisisitiza uamuzi huo katika
kikao hicho cha ndani Ndugu Polepole alisema Kama mtumishi wetu namba
moja kwenye Chama na Serikali yetu Ndugu John Pombe Joseph Magufuli
anajua kuwa cheo ni dhamana, wewe mwingine unapata wapi nguvu ya kutumia
cheo kwa faida yako
Akitoa neno la kuhitimisha Ndugu
Humphrey Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinafanya mageuzi
makubwa ya kurejesha chama kwa wanachama, kusimamia rasilimali za chama
zitumike kwa manufaa ya chama, kujenga misingi imara ya utoaji haki
ndani ya chama pamoja na kuhakikisha katika chaguzi zinazoendela CCM
inapata viongozi wenye sifa “Haipaswi wakati wowote kugeuza Chama hiki
kuwa chama cha viongozi, Chama hiki tangu awali msingi wa kuanzishwa
kwake ni kuwa kiwe chama cha wanachama na kinachoshughulika na shida za
watu
Pia Ndugu Polepole amempokea na
kuagiza uongozi wa ngazi ya tawi kumpokea na kumpa mafunzo ya Itikadi ya
Chama Cha Mapinduzi(CCM) aliyekuwa mgombea udiwani na Mwenyekiti wa ACT
kata Kidatu Ndugu Deodatus Makolo ambaye leo amejivua nafasi zake zote
za uongozi katika chama hicho na kujiunga na CCM.
Ndugu H.H. Polepole yupo ziarani
Mkoa wa Morogoro, kukagua na kujionea zoezi la uchaguzi wa ndani ya
Chama ngazi ya msingi unaoendelea, kipindi hichi ambacho CCM inafanya
mageuzi makubwa ya kiuongozi, kimuundo na kiutendaji. Ziara hii ni
muendelezo wa ziara za kichama na vikao vya ndani vyenye lengo la kutoa
hamasa, kuvumisha umuhimu wa Mageuzi ya Chama, kuimarisha Chama na
kutatua kero za wanachama.
SHARE
No comments:
Post a Comment