Winga
mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars aliyekuwa
anaichezea Dar es Salaam Young Africans Simon Msuva ametangazwa kujiunga
na club ya Difaa El Jadida ya Morocco.
Simon
Msuva amejiunga na club hiyo ikiwa ni siku mbili zimepita toka aondoke
Tanzaniakwenda kujiunga na club hiyo, Msuva sasa anaungana na Ramadhani
Singanoaliyekuwa anaichezea Simba na Azam FC katika club ya Difaa El
Jadida.
Kutoka kulia Dr Tiboroha ambaye ni meneja wa Simon Msuva wakiwa na viongozi wa Difaâ El Jadidi
Msuva
amepata nafasi ya kujiunga na Defaa El Jadida kwa mkataba wa miaka
mitatu na tutamuona katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika
akiichezea El Jadida ambayo imemaliza msimu ikiwa nafasi ya pili nyuma
ya Wydad Casablanca kwa tofauti ya point saba.
SHARE
No comments:
Post a Comment