Mke wa
Rais wa Zimabwe, Robert Mugabe, Grace Mugabe amemtaka kiongozi huyo
kumtangaza mrithi wake wa urais ili kuondoa minong’ono kuhusu mtu
atakayemrithi akiondoka madarakani.
”Rais
hafai kuwa mwoga kumchagua mrithi wake na neno lake litakuwa la mwisho”,
alisema Bi Grace Mugabe.Rais Mugabe ndio kiongozi mzee zaidi duniani na
chama chake cha ZANU PF kimemchagua kuwania urais kwa mara nyingine
mwaka ujao.
Lakini
makundi ya wapinzani yamekuwa wakijipanga kuwania urais ili kuimarisha
uwezo wao huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali yake ya kiafya.
Chanzo: BBC Swahili
SHARE
No comments:
Post a Comment