Kampuni
ya Mantrac Tanzania imezindua mpango maalum wa kukodisha na kumiliki
mitambo kwa kulipa kidogo kidogo ili kuwarahisishia wateja mzigo wa
kulipa fedha kununua mtambo kwa mara moja.
Hii
inamaanisha kuwa wafanyabiashara na wakandarasi wataweza kukodisha
mitambo kutoka katika kampuni ya Mantrac Tanzania kwa bei nafuu na
kuanzia miezi sita na kuendelea anakuwa mmiliki kamili wa mtambo huo.
Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha mipango na masoko Bw Valence Pantaleo. Alisema
katika kipindi chote cha kukodisha, kampuni ya Mantrac Tanzania
inagharamia matengenezo ya mtambo huo kadiri ya mwongozo wa kampuni ya
CAT.Mpango
wa kukodisha na kumiliki ni maalum ambao unamwezesha mkandarasi au
mfanyabiashara kupata manufaa lukuki ya kutumia mitambo inayotumia
tekinolojia ya kisasa kabisa ya kampuni ya CAT bila ya kununua mtambo
huo mwanzo wa mradi.
Mpango huu unatoa unafuu mkubwa sana na huweza kupunguza sana gharama za uendeshaji kwa mkandarasi au mfanyabiashara.
Kampuni
ya Mantrac Tanzania inamhakikishia mteja mitambo na tekinolojia
madhubuti ya Catepillar yenye historia pana ya kutengeneza na kuuza
mitambo ya kisasa inayotumia katika miradi mikubwa ya kujenga
miundombinu.
Miradi hii mikubwa ya miundombinu ni pamoja na ujenzi wa barabara, reli, majengo, madaraja, kwenye madini na kilimo.
Bidhaa
zinazouzwa na kampuni ya Mantrac Tanzania zinapatikana katika matawi
mbalimbali nchini kama vile Dar es Salaam, Mtwara, Mwanza, Mbeya, na
Kilimanjaro.Bw Pantaleo alisema baada ya kupata mafanikio makubwa katika biashara kati ya kampuni ya Mantrac Tanzania na wateja kwenye
mitambo
mipya, iliyotumika na kukodisha mitambo, sasa kampuni imeamua kuleta
mpango huu wa kukodisha na kumiliki ambapo mteja atalipa kidogo kidogo
hadi pale atakapomiliki mtambo wake.Alisema
kamupuni ina mitambo mingi inayofikia zaidi ya dola za kimarekani
milioni 15 kwa ajili ya kutekeleza mpango huu mpya wa kukodisha na
kumiliki.Kampuni
ya Mantrac Tanzania ndio pekee yenye kibali cha kusambaza na kuuza
mitambo mbalimbali inayotengenezwa na kampuni ya CAT hapa nchini
Tanzania.
Kampuni
pia ina vituo maalum vya huduma kwa ajili ya matengenezo ya mitambo,
ina wataalamu wa hali ya juu na vifaa vyenye viwango vya kimataifa
ambavyo hutumika katika kuchunguza tatizo na kutengeneza ubovu
unaojitokeza katika mitambo.
Katika mpango huu, vigezo na masharti vitazingatiwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment