MWIGIZAJI wa Bongo Muvi, Yusuf Mlela amesimulia
mazingira yote ya namna alivyonusa kifo, kufuatia ajali aliyoipata hivi
karibuni iliyosababisha kulazwa hospitalini kwa siku kadhaa.
Mlela aliliambia Wikienda kuwa,
alipata ajali hiyo ya gari huko Mombasa nchini Kenya, majira ya usiku
alipokuwa akielekea klabu kuhudhuria shoo ya wasanii kutoka Bongo, Ben
Pol na G-Nako, baada ya gari alilokuwa akitumia na rafiki zake kupoteza
mwelekeo na kugonga kalavati na kuviringika mara mbili, hivyo akapoteza
fahamu na kuchanika sehemu ya juu ya mdomo ambapo alipozinduka akajikuta
hospitalini.
Mlela
alisema kuwa, waliondoka nyumbani kwa mwendo wa kawaida, lakini wakiwa
njiani gari lilianza kuyumba na baadaye dereva kushindwa kulidhibiti
hivyo kuparamia ukingo wa kalavati hilo.
“Ninamshukuru
sana Mungu kwa kuninusuru na roho ya kifo vinginevyo sasa stori
ingekuwa tofauti kabisa, ajali isikie kwa wengine, nashangaa hata huu
mdomo umeponaje na kurudia hali yake ya kawaida maana ulichanika ile
mbaya,” alisema Mlela.
SHARE
No comments:
Post a Comment