Kura
zimekwishapigwa nchini Senegal huku televisheni ya umma ikiripoti kuwa
asilimia 54 ya raia wa nchi hiyo wamejitokeza kupiga kura.
Polisi imesema wajumbe watatu wa muungano wa Bwana Wade walikamatwa kwa kufanya vurugu kwenye vituo vya kupigia kura.
Rais Sall anatafuta wingi wa viti katika chama chake.
Abdoulaye Wade amethibitisha kuwa muunngano wa vyama vidogo vidogo unamuandaa mtoto wake wa kiume Karim kuwania urais mnamo mwaka 2019.
Mgombea mwingine ni meya wa mji mkuu wa Senegal , Dakar, ambaye yuko gerezani kwa mashtaka ya ubadhilifu wa mali ya umma. Matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa Jumatatu asubuhi.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment