MSANII wa Bongo Flava na mtangazaji wa Choice FM, Feza Kessy, amesema kutokana na kazi yake ya utangazaji kuna baadhi ya vyombo vya habari nchini vimekuwa havimpi sapoti yoyote.
Mwimbaji
huyo amedai kuwa kabla ya kuingia katika utangazaji mambo yalikuwa
tofauti na sasa na hivyo ameviomba vyombo hivyo vya habari vitenganishe
kazi yake na muziki.
“Kwa
mfano mimi kuwa CMG kuna media zinaniogopa, sijui wanavyowaza wao
lakini sapoti inakuwa inapungua. Ningependa ile sapoti ya muziki
iendelee kama walivyokuwa wanafanya mwanzo. Sasa hivi wamepunguza kasi
kwani kuna sehemu hata ‘interview’ nabaniwa,” ameiambia XXL ya Clouds FM na kuongeza:
“Kuna
media nyingine wanacheza muziki wangu lakini kuna ‘specific media’
ambazo hata ‘interview’ nilishindwa kupata. Siwezi kuzitaja kwa sasa
hivi ila wajue ‘this is business’, ni kazi yangu ‘as an individual’
wasini-judge kikampuni,” amesisitiza.
Feza
Kessy kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa ‘Kaa Kijanja’
ambao amemshirikisha rapa kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili.
SHARE
No comments:
Post a Comment