Taasisi
ya MO Dewji Foundation inayojuhusisha na kusaidia jamii katika elimu,
afya na maendeleo ya jamii imetunukiwa tuzo ya kimataifa ya ubora
inayofahamika kama SuperBrand. Taasisi
hiyo inayomilikiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohammed
Entreprises Tanzania Limited, Mohammed Dewji imetunukiwa tuzo hiyo
kutokana na juhudi zake za kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali
ambayo inaifanya.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji,
Barbara Gonzalez amesema ni heshima kubwa kwa taasisi kupata tuzo hiyo
lakini pia itawasaidia kufanikisha miradi mikubwa ambayo wamepanga
kuifanya na taasisi kubwa kama ya Bill Gates.
“Kwa niaba ya Taasisi ya MO Dewji na kampuni ya MeTL Group tunashukuru sana kwa tuzo hii na huu ni mwanzo mpya wa safari yetu, kama mnavyojua taasisi yetu ilianzishwa mwaka 2014 na katika kipindi cha miaka miwili tumeanzisha miradi mbalimbali kama MO Entrepreneurs na MO Scholars ikiwa na lengo la kuwasaida vijana na tunafuraha Baraza la SuperBrands limetutambua.
“Tuzo
hii inatusaidia katika miradi mikubwa kwa sasa kama taasisi ya Mohammed
Dewji tunataka kufanya ushirikiano na taasisi kubwa kama Taasisi ya
Bill Gates, kushirikiana na taasisi za Kenya, Uganda, UK, jina la
Mohammed Dewji litakuwa la kwanza na SuperBrand litakuwa ya
pili,” amesema Barbara. .
|
Mkurugenzi
wa taasisi huru ya Superbrands Ukanda wa Afrika Mashariki, Jawad Jaffer
akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez
tuzo ya ubora ya SuperBrand.Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo ya ubora ya SuperBrand.
|
Tuzo ya SuperBrand ambayo Taasisi ya MO Dewji imetunukiwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment