Msanii
wa Bongo Flava chini ya label ya PKP, Nedy Music amesema si kweli kuwa
haelewani na Dogo Janja bali alikuwa anamuelekeza baadhi ya mambo.
Miezi
miwili iliyopita Nedy Music aliiambia Bongo5, “nachoweza kusema ni
kwamba Dogo Janja asaidiwe, ana zeeka vibaya kila siku anabadilika,
uwezo wake wakufikiri unapungua kila siku”. Kauli hiyo ilikuja baada ya
Dogo Janja kutamba yeye ndiye msanii anayeongoza kwa kuvaa vizuri Bongo.
Sasa
leo hii Nendy Music akizungumza na Daladala Beats ya Magic Fm amesema
alikuwa akimuelekeza Dogo Janja kama mdogo wake na sasa ameanza kuelewa.
“Dogo
janja tunaongea tena ni washikaji kabisa, ni vitu vidogo nilikuwa
namuelekeza mdogo wangu na si vibaya akawa ananisikiliza na hatimaye
ananisikiliza naona kidogo kidogo anapanda,” amesema Nedy Music.
SHARE
No comments:
Post a Comment