MSANII
wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amebadili jina lake na kujiita
Nisha Minhal Azad huku kisa kikidaiwa kuwa amefanya hivyo baada ya
kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na ‘Serengeti Boy’ anayetumia jina
hilo.
Kwa
mujibu wa chanzo cha karibu na msanii huyo, Nisha amekuwa karibu na
‘Serengeti Boy’ huyo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva na kwamba
ameamua kuanika kabisa uhusiano huo bila kificho.
“Nisha amepata tulizo baada ya kukaa
kwa muda mrefu bila kuwa na mwanaume. Huyo mpenzi wake wa sasa ni msanii
wa Bongo Fleva anajulikana kwa jina la Minu, yaani Nisha humuelezi
chochote juu ya dogo huyo na wanaongozana mara kwa mara,” kilidai chanzo
na kuongeza;
“Kwa
sasa ameamua kuanika ukweli huo kila kona, kwenye mitandao ya kijamii
amebadilisha mpaka jina lake na kujiita Nisha Minhal Azad. Hivi karibuni
aliweka picha katika Insta yake akiwa naye katika pozi la mahaba na
kuandika; ‘kuna tofauti kubwa kati ya Serengeti na Ngorongoro.’
Baada
ya kunasa madai hayo, Ijumaa lilimtafuta Nisha na kumuuliza ukweli juu
ya kinachoonekana na kuongelewa, alipopatikana alikiri kubadili jina na
kuwa katika uhusiano na Serengeti Boy huyo;
“Ni kweli nipo katika uhusiano na huyo mtu, mengine siwezi kuyaanika ila kifupi ni hivyo.”
Nisha
kwa nyakati tofauti aliwahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na staa
wa Bongo Fleva, Emmanuel Elbariki ‘Nay wa Mitego’ pamoja na Baraka
Andrew ‘Barakah The Prince’.
SHARE
No comments:
Post a Comment