Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akikabidhi kadi kwa mmoja wa watoto waliojiunga na bima ya afya ya
watoto (TotoAfyaCard) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
salaam leo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Taifa ya
Afya (NHIF) Spika Mstaafu Mama Anne Makinda na kushoto ni Benarld Konga
Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa (NHIF).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akikata utepe wakati alipozindua bima ya watoto (TotoAfyaCard) kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
…………………………………………..
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
amezindua (TotoAfyaKadi) Bima ya Afya kwa watoto. katika uzinduzi
uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam aki,
Kwa mujibu wa Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), kati ya Watanzania 52m
waliopo sasa (2017) watoto ni 26.7m (sawa na 51%). Mtoto ni mtu mwenye
umri wa chini ya miaka 18.
Ummy Mwalimu anasema (TotoAfyaKadi) ni njia sahihi ya
kuelekea Bima ya Afya kwa Wote nchini. Mpango huu unatoa Uhakika wa
Matibabu kwa mtoto kwa Tshs 50,400/= kugharamia matibabu yake kwa mwaka
mzima. Tena sio kwa Vituo vya Serikali bali pia vya Binafsi. Lakini pia
si kwa Halmashauri au Mkoa unayoishi bali nchi nzima.
Waziri Ummy Mwalimu ameongeza kusema “Wazazi na Walezi
wenzangu Ugonjwa huja bila Taarifa! Tuchangamkie (TotoAfyaKadi) ili
kuwa na uhakika wa matibabu ya Mtoto kabla ya kuugua kwani Mwenye Macho
haambiwi Tazama. (TotoAfyaKadi) ndio mpango mzima.
SHARE
No comments:
Post a Comment