Polisi wawili wa
Israeli wamefariki baada ya Waisraeli watatu wa asili ya Kiarabu
waliokuwa na silaha kuwamiminia risasi katika eneo la mji wa kale wa
Jerusalem.
Afisa mwingine wa polisi alijeruhiwa.
Msikiti wa al-Aqsa, umefungwa na watu kuhamishwa.
Sala ya Ijumaa iliyopangiwa kufanyikia huko, imefutiliwa mbali kwa mara ya kwanza kwa miaka mingi.
Waziri wa usalama wa Israel, amesema kuwa, washambuliaji hao "walivuka mpaka".
Eneo hilo la kale la mji lipo katika maeneo ya Mashariki mwa Jerusalem, maeneo yaliyotwaliwa na Israel katika vita vikali vya mwaka 1967- hatua ambayo haitambuliwi na mataifa ya Dunia.
Kumekuwepo na msururu wa visa vya watu kuchomwa visu na wengine kukanyagwa au kugongwa kwa magari tangu mwaka 2015, walengwa sana wakiwa Waisraeli.
Mashambulio hayo hutekelezwa na Wapalestina au Waarabu Waisraeli. Washambuliaji waliotekeleza mashambulio ya awali walikuwa wa asili ya Jordan.
Polisi wanasema wasahmbuliaji waliowashambulia polisi hao walikuwa na umri wa kati ya miaka 19 na 29 na walitoka mji wa Umm al-Fahm, kaskazini mwa Israel.
Shirika la usalama la Israel la Shin Bet limesema awali hawakuwa wanafahamika au kufuatiliwa na maafisa wa usalama.
SHARE
No comments:
Post a Comment