Gavana wa jimbo la
Nigeria anasema kuwa anatarajia Rais Muhammadu Buhari kurudi nyumbani
kutoka Uingereza katika kipindi cha wiki mbili zijazo.
Kutokuwepo kwake kumezua hali ya wasiwasi nchini Nigeria, huku watu wakidai kwamba huenda amefariki.
Wengine wamekuwa na wasiwasi kwamba huenda asirudi tena.
Baadaye afisi ya rais ilitoa picha za Buhari mwenye umri wa miaka 74 akikutana na magavana kutoka chama chake.
Ni mara ya kwanza amepigwa picha mjini London tangu aondoke Nigeria yapata siku 80 zilizopita.
Gavana wa jimbo la Imo aliambia BBC siku ya jumatatu kwamba'' nilikutana na mtu mwenye motisha na anendelea vyema.
Hajapoteza ucheshi wake kama anavyojulikana. Kwa hivyo anaendelea vyema na tunafurahi sana kumuona na tunadhani amefanya kitu muhimu kuwahakikishia raia wa Nigeria kuhusu afya ya rais wao''.
Bwana Okorocha awali alisema kwamba bwana Buhari alipuuzilia mbali uvumi kuhusu afya yake alipoulizwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment