Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameahidi kuendeleza vita dhidi ya
biashara ya dawa za kulevya, huku akiwapuuza wakosoaji ambao anasema
wanapunguza umuhimu wa kampeni yake kwa kisingizio cha kutetea haki za
binaadamu na kuwalaumu maafisa kwa kusababisha umwagaji damu.
Duterte ameitumia hotuba yake kwa taifa kuutetea msako dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya ambao umesababisha vifo vya maelfu ya Wafilipino.
Amesema ijapokuwa anathamini maisha ya binaadamu, anahitaji kupambana na wanaojinufaisha na watu wanyonge na kuzuia uwekezaji wa kigeni nchini humo.
Msako dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya ndio kampeni inayouelezea utawala wa Duterte na imesababisha shutuma za kimataifa, ambapo makundi ya haki za binadamu yanamkosoa kwa kufanya kampeni ambayo kwa kiasi kikubwa inawalenga watumiaji wa dawa za kulevya kutoka jamii maskini na kutowagusa vigogo wa biashara hizo.
CHANZO: DW

No comments:
Post a Comment