TRA

TRA

Tuesday, July 25, 2017

Urusi yapeleka Polisi eneo salama Syria

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Rais wa Urusi, Vladmir Putin 

Urusi imepeleka jeshi la polisi kufuatilia mpango wa kusitishwa mapigano katika ukanda salama wa viunga vya mashariki mwa mji mkuu wa Syria, Damascus. 

Mkuu wa jeshi wa Urusi Kanali Jenerali Sergei Rudskoi amesema kuwa Urusi imeweka vituo viwili vya ukaguzi na vituo vinne vya uchunguzi katika moja ya maeneo salama, ya Ghouta Mashariki. 

Wizara ya Ulinzi ya Urusi wiki iliyopita ilisema kuwa serikali ya Syria na upinzani zilifikia makubaliano kuhusu mipaka ya ukanda huo, siku kadhaa baada ya mashambulizi ya ardhini na angani kulikumba eneo hilo. 

Urusi imekuwa ikitoa msaada wa mashambulizi ya angani kwa Rais wa Syria Bashar al-Assad katika vita vyake dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS tangu mwaka wa 2015 na hapo awali ilipeleka jeshi la polisi kuweka doria katika mji wa Aleppo mwaka jana. 

CHANZO: DW

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger