Wizara ya elimu
nchini Sudan imeripotiwa kutoa agizo kwa shule zote za kanisa kufunga
siku ya Ijumaa na Jumamosi na kuendelea na masomo kama shule nyingine
siku ya Jumapili.
Kanisa linalalamika kwamba siku ya Jumapili imekuwa siku huru ya shule za kanisa tangu shule hizo zianzishwe nchini humo.
Kulingana na Wakristo Jumapili ni siku ya kupumzika wakati ambapo Waislamu hupumzika siku ya Ijumaa.
Hatua hiyo inajiri muda mchache kabla ya kiongozi wa kanisa Anglikana duniani kutembelea Sudan
SHARE
No comments:
Post a Comment