Msanii
wa Bongo Fleva ambaye haishiwi vituko, Harmorapa amekunwa na utendaji
kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe
Magufuli wa kubana fedha kitu ambacho kimewafanya watanzania kutumia
pesa kwa nidhamu.
“Kwanza mimi nimpe tu pongezi kwa sababu amefanya watu wengi sana wajue
kuhangaika na wajue kufanya kazi tofauti na kipindi cha nyuma watu
walikuwa wazembe”,amesema Harmorapa baada ya kuulizwa swali la kuhoji
utendaji kazi wa Rais Magufuli kwenye kipindi cha Twenzetu cha Times FM.
Harmorapa amesema kipindi hiki cha awamu ya Rais Magufuli kimewafanya
watanzania kuithamini pesa ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi yasiyo
na ulazima kitu ambacho ni tofauti kabisa na kipindi cha nyuma.
Hata hivyo, Harmorapa amesema awamu hii ya tano Serikali imekuwa
ikihimiza sana vijana kufanya kazi kuliko kuendekeza starehe kitu
ambacho kimewafanya vijana wengi kujituma na kupata molali ya kufanya
kazi.
SHARE
No comments:
Post a Comment