Na Tamimu Adam - Jeshi la Polisi.
Jeshi
la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni
miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika Kanda maalumu ya
kipolisi Rufiji ambapo mmoja kati ya watu hao ametambulika kwa jina la
Abdallah Ally Ngande Makeo ambaye alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi
kwa muda mrefu kutokana na kushiriki kwake katika matukio ya mauaji
maeneo ya Ikwiriri, Kibiti pamoja na uvamizi wa kituo cha Polisi
Ikwiriri.
Akielezea
tukio hilo, Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu
Kamishna wa Polisi, Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea
mnamo tarehe 19 Julai, 2017 saa mbili usiku katika eneo la Utende kata
ya Ikwiriri, wilaya Rufiji kanda maalum ya Polisi Rufiji.
“
Askari Polisi wa doria waliwatilia mashaka watu wanaokadiliwa kuwa
watano ambapo walianza kuwafutilia ndipo walianza kukimbia huku
wakiwashambulia askari kwa risasi, askari nao kwa ujasiri walijibu
mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi wahalifu wawili miongonio mwao
ambao baadaye walifariki wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya muhimbili
kutokana na kuvuja damu iliyosababisishwa na majeraha ya risasi
waliyoyapata” alisema Sabas.
Aliongeza
kuwa katika eneo hilo la tukio ilipatikana silaha moja aina ya rifle
375 ambayo ilikutwa imekatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi mbili (2).
Aidha, Miili ya marehemu wote wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia
maiti hospitali ya Taifa ya muhimbili.
Kamanda Sabas ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na
Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa wahalifu
wengine waliosalia na kwamba opereheni hiyo ya kuwasaka wahalifu katika
Kanda hiyo ya kipolisi Rufiji ni endelevu na hakuna atakaye baki.
Mkuu
wa Operesheni Maalun za Jeshi la Polisi, Naibu kamishina wa Polisi
(DCP) Liberatus Sabas akiwa katika eneo la tukio akizungumzia namna
Jeshi la Polisi lilivyofanikiwa kuuawa watu wawili awanaosadikiwa kuwa
ni miongoni mwa wahalifu wanaojihusisha na mauaji watu katika Ikwiriri
na kibiti. (Kushoto kwake ) ni Kamanda wa Kanda maalum ya Kipolisi
Rufiji, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Onesmo Lyanga
akiwa ameshika silaha aina ya Rifle 375 iliyokutwa katika eneo la tukio.
Picha na Tamimu Adam.
SHARE
No comments:
Post a Comment