Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akiwaeleza wananchi wa Kijiji cha Kiangala jinsi serekali ya awamu ya
tano inavyo shughulikia kero za za wananchi Nchini Wananchi hao
walijitokeza Julai 10, 2017 ili waweze kumueleza kero zinazo wasumbua
Waziri yupo Wilayani Liwale Mkoa wa lindi Kwaziara ya Kikazi ya siku
Nne
………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema Serikali haitahusika na ulipaji wa deni la fedha za Ushirika na
badala yake kila aliyekula fedha hizo atazilipa mwenyewe.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo
(Jumatatu, Julai 10, 2017), wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya
Liwale katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa
wilaya.
Waziri Mkuu ambaye yuko katika na
ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, amesema Serikali haiwezi
kukubali Ushirika ukafa nchini kwa ajili ya watu wachache wasiokuwa
waaminifu.
Amesema watu wote waliopewa dhamana ya kuongoza Vyama vya Ushirika na kuamua kujinufaisha kwa kula fedha za vyama watazilipa.
Waziri Mkuu amewaagiza Viongozi
wa Mkoa wa Lindi kufanya ukaguzi katika Vyama vyote vya Ushirika vya
Msingi (AMCOS) ili kubaini ni wakulima wangapi wanadai.
Amesema baada ya kufanya
uchunguzi na kubaini idadi ya wakulima wanaodai na kiasi cha fedha
wawachukulie hatua wahusika wote kwa mujibu wa sheria.
Awali, Waziri Mkuu alizungumza na
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale katika Ukumbi wa
Tengeneza, ambapo amewataka Watumishi wa Umma Nchini kutojihusisha na
vitendo vya rushwa katika utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Amesema Watumishi wanawajibu wa
kuwahudumia Wananchi bila ya kutengeneza mazingira ya kuomba rushwa na
atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Amesema Watumishi wa Umma
wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya
kiutumishi jambo litakaloondoa malalamiko kutoka kwa Wananchi.
“Lazima Wananchi waone na
wanufaike na kazi inayofanywa na Serikali yao, hivyo ni wajibu wa
Watumishi kuwatumikia Wananchi popote walipo na si kukaa maofisini.”
Pia amewataka Watumishi hao kupanga mipango itakayoleta tija kwa Wananchi na si vinginevyo
SHARE
No comments:
Post a Comment