Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kufunga
mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani
Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ladislaus Mwamanga akizungumza wakati wa
kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka
huu. Mafunzo hayo yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango
mkoani Dodoma.
Mmoja wa Wadadisi Maro D. Maro
akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi wa Utafiti
wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo yamefungwa
leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wadadisi na Wasimamizi
wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi
wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo
yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wadadisi na Wasimamizi
wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi
wa Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo hayo
yamefungwa leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma. (PICHA
ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)
……………………………………………………………………………………..
Na: Veronica Kazimoto-Dodoma
WITO
umetolewa kwa viongozi wa Serikali na wananchi kwa ujumla kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa Wadadisi watakaopita maeneo mbalimbali nchini
kukusanya taarifa kwa ajili ya Utafiti wa Awamu ya Pili wa Kutathmini
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka
huu.
Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya Wadadisi wa utafiti huo
iliyofanyika leo mkoani Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ladislaus Mwamanga amesema utafiti huo ni
muhimu katika kunusuru kaya maskini nchini hivyo haina budi viongozi na
wananchi kutoa ushirikiano kwa Wadadisi wa utafiti husika.
“Kwa
namna ya pekee nawaomba Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya, Wakurugenzi
wa Manispaa na Halmashauri, viongozi wa kata na vijiji na wananchi wote
kwa pamoja mtoe ushirikiano wa hali ya juu kwa Wadadisi watakapokuwa
katika maeneo yenu wakikusanya taarifa za utafiti huu”, amesema
Mwamanga.
Nae
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema
lengo la kufanya mafunzo hayo ilikuwa ni kuwawezesha Wadadisi kufahamu
taratibu zote zinazohusu kazi ya ukusanyaji taarifa na mbinu
zinazotakiwa ili kupata taarifa sahihi kutoka kwenye kaya mbalimbali
nchini.
Jumla
ya Wadadisi 85 wamemaliza mafunzo ya siku 20 ya Utafiti wa Awamu ya
Pili wa Kutathmini Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini yaliyoandaliwa na
Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na TASAF.
SHARE
No comments:
Post a Comment