KAMPENI
ya Uzalendo Kwanza iliyoanzishwa na Wasanii wa Filamu nchini, a.k.a
Bongo Muvi inazidi kupanua wigo wake baada ya kuongeza matawi yake kwa
mikoa yote ya Tanzania huku ikipata wanachama wakongwe waliowahi kutamba
ndani ya Soka hapa nchini.
Akizungumza
na wanahabari wakati akiwapokea wanachama wapya, Mwenyekiti wa Chama
hicho, Steve Mengele 'Steve Nyerere' amesema kuwa, lengo la Chama hicho
ni kuwafikia Watanzania wote kufahamu umhimu wa uzalendo, kuipenda nchi
yako ikiwa ni pamoja na kushirikiana kikamilifu na Serikali ya awamu ya
tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kumuunga mkono wa kizalendo
katika kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kimaendeleo.
"Taifa
la wazalendo linaanzia darasani, tunawaomba walimu wote wawe wazalendo
kufundisha darasani, manesi na madakatari wawe wazalendo kutoa huduma
zao, uzalendo pia ni mhimu kusapoti vilabu vyetu vya soka na Timu ya
Taifa,na Wasanii wetu wa muziki ni lazima wawe wazalendo kwa kuitangaza
nchi yao kwa mambo ya Kizalendo," alisema Nyerere.
Wacheza
soka ambao wamejiunga na Uzalendo Kwanza ni; Mwanamtwa Kihwelo, Monja
Liseki, Abdallah Kaburu, Dotto Mokili na wengine.Aidha Nyerere amewaasa
wanachama hao na Watanzania wote kuunganisha nguvu ya pamoja ili kulinda
kazi zao za sanaa sambamba na kuwafanya Watanzania kupenda vilvivyo
vyao mfano, kazi za wasanii wa ndani ili kukuza kipato chao na kuinua
uchumi wa nchi.
Mbali
na hao, msanii wa Bongo Fleva, atambulikae kwa jina la Ruby pia
amejiunga na kampen ya Uzalendo Kwanza,Msanii huyo amepewa jukumu la
kutunga nyimbo za Uzalendo na video zake ili kufikisha ujumbe kwa
wananchi wote.
Katika
hatua nyingine,Uongozi wa Uzalendo kwanza umetoa msaada wa vyakula
mbalimbali na kiasi cha fedha tasilimu Laki tano kwa aliyewahi kuwa
mpiga picha wa Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News),Athuman
Hamis ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa
kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea
kwa tukio hilo.
Steve
Nyerere amemaliza kwa kuwaasa Wasanii wenzake kuendelea kuwa Wazalendo
na kuwakumbusha kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya kijamii,amesema
kuwa mfuko wa hifadhi ya Jamii PPF wameanza kwa kuidhamini kampeni yao
ya Uzalendo Kwanza,huku wakionesha utayari mkubwa wa kuwasaidia iwapo
wataamua kuendelea kujiunga katika mfuko huo na ukawa mkombozi kwao.
Mmoja
wa Mabalozi wa Kampeni ya Uzalendo Kwanza akiwasili kwenye
mkutano,Athuman Hamis aliyewahi kuwa mpiga picha wa Magazeti ya Serikali
(Habari Leo &Daily News), ambaye alipata ulemavu wa kudumu kufuatia
ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku yake ya Kazi ikiwa yapata miaka
kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.
Mwenyekiti
wa kampeni ya Uzalendo kwanza Steve Mengele almaarufu kwa jina la Steve
Nyerere akimkabidhi bahasha yenye kiasi cha fedha shilingi laki tano
pamoja na msaada wa vyakula mbalimbali kwa aliyewahi kuwa mpiga picha wa
Magazeti ya Serikali (Habari Leo &Daily News),Athuman Hamis ambaye
alipata ulemavu wa kudumu kufuatia ajali aliyoipata akiwa kwenye majuku
yake ya Kazi ikiwa yapata miaka kumi sasa tangu kutokea kwa tukio hilo.
Mwenyekiti
wa kampeni ya Uzalendo kwanza Steve Mengele almaarufu kwa jina la Steve
Nyerere akimnyanyua Mzee Rajab Shabani mkazi wa Mburahati ambaye ni
mlemavu wa miguu (kwa miaka mitano sasa),kumkalisha kwenye kiti cha
matairi matatu (Wheel chair),ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na
Wadau wa kampeni hiyo wakishirikiana na uongozi wa kampeni ya Uzalendo
kwanza.
Pichani
kati ni Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo Kwanza , Steve Mengele 'Steve
Nyerere' akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini
dar,wakati akiwapokea wanachama wapya walioamua kujinga na kampeni
hiyo.Pichani kulia ni Mjumbe Halima Yahya na kushoto ni Misayo
Ndumbagwe.
Pichani
kati (njano) Mwenyekiti wa kampeni ya Uzalendo Kwanza , Steve Mengele
'Steve Nyerere' akiwatambulisha wanamichezo wazalendo wa zamani katika
Soka na Waigizaji wengie mahiri mbele ya Waandishi wa habari mapema leo
jijini dar,walioamua kujiunga na kampeni hiyo ya Uzalendo Kwanza.
Pichani
Kati ni Msanii wa bongofleva Hellen Majeshi a.k.a Ruby ambaye pia
ametangazwa kujiunga na kampeni hiyo ya Uzalendo Kwanza.
Baadhi
ya Wasanii mbalimbali wa Bongo movie wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri
kwenye mkutano huo na Waandishi wa Habari uliofanyika mapema leo,jijini
Dar.
SHARE
No comments:
Post a Comment