Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la
Kujenga Taifa Msange (823 KJ) Luteni Kanali Mohammed Mketto alitoa
taarifa jana mjini Tabora ya mafunzo ya vijana waliohitimu kwa mujibu wa
Sheria kuwa waliingia kambi hapo wakiwa 1543 na wamefanikiwa kumaliza
mafunzo yao wote.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Queen
Mlozi akimkaribisha jana mjini hapa Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ili afunge mafunzo kwa mujibu wa
sheria ambayo yanajulikana kama Opereshi Tanzania ya Viwanda
yaliyofanya katika Kikosi cha Jeshi cha 823 JKT Msange
Mkuu wa Bregedi ya 202 kundi la
Vikosi vya Kanda ya Magharibi (FARU) Brigedia Jenerali Stephen Mkumbo
alitoa nasaha kwa wahitimu wa JKT juu ya kuwa mabalozi wa masuala ya
ulinzi na usalama katika maeneo yao ili Tanzania iendelee kuwa kisiwa
cha amani jana mjini Tabora wakati ufungaji wa mafunzo ya Opereshi
Tanzania ya Viwanda katika Kikosi cha Jeshi cha 823 JKT Msange.
Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la
Kujenga Taifa chini (JKT) Brigedia Jenerali Elizaphania Marembo
akihutubia jana mjini Tabora juu ya wahitimu wa mafunzo ya JKT Msange wa
Opereshi Tanzania ya Viwanda kujiepusha na Wanaharakati watakapokuwa
katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwani wapo ambao lengo lao ni
kuhakikisha nchi inavurugika na Watanzania wanagawanyika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama Mkoa na ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri
akikagua Gwaride rasmi la kufunga mafunzo wa vijana wa Jeshi la Kujenga
Taifa kwa mujibu wa sheria ambayo yanajulikana kama Opereshi Tanzania
ya Viwanda katika Kikosi cha Jeshi cha 823 JKT Msange yaliyofanyika
jana wilayani Tabora.
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye koti jeusi) akiwa na
viongozi mbalimbali wa JWTZ na wageni wengine waalikwa wakifuatilia
burudani wakati wa sherehe za kuhitimu mafunzo ya JKT kwa mujibu wa
sheria ambayo yanajulikana kama Opereshi Tanzania ya Viwanda yaliyofanya
katika Kikosi cha Jeshi cha 823 JKT Msange jana wilayani Tabora.
Wahitimu wa Mafunzo ya Mujibu wa
sheria Opereshi Tanzania ya Viwanda wakila kiapo cha Utii wa Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Rais wa Jamhuri
wa Muungano wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika jana mjini Tabora
katika Kikosi cha Jeshi cha 823 JKT Msange.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama Mkoa na ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri
akitoa hotuba jana mjini hapa katika sherehe za kufunga mafunzo wa
vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa sheria ambayo
yanajulikana kama Opereshi Tanzania ya Viwanda katika Kikosi cha Jeshi
cha 823 JKT Msange jana wilayani Tabora.
……………………………………………………………….
Na Tiganya Vincent-RS_Tabora
WAHITIMU wa Mafunzo ya Mujibu wa
Sheria Operesheni ya Tanzania ya Viwanda wametakiwa kutumia elimu
waliyopata katika kuhakikisha kuwa wanakuwa wazalendo na watiifu kwa
wananchi na Serikali yao ili kuhakikisha kuwa nchi hii haingiliwa na
adaui yoyote kwa makusudi ya kuvuruga amani iliyopo.
Kauli hiyo imetolewa na
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na ambaye ni Mkuu wa Mkoa
wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri jana wilayani Tabora wakati akifunga
mafunzo wa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Opereshi Tanzania ya
Viwanda katika Kikosi cha Jeshi cha 823 JKT Msange.
Alisema kuwa ni vema wakatumia
mafunzo waliopatiwa katika kuwafichua wale wote wenye nia mbaya ambao
wanaishi katika jamii zao wanapoishi na wale wanaoingia nchi kwa njia za
panya ambao wanakusudia kuendesha vitendo vinavyohatarisha umoja wa
Watanzania.
“Maadui wamebadili medani za
kufanya uhalifu …ni vema mkatumia mafunzo hayo mliopatiwa na makamanda
wetu kuwafichua watu wenye nia ovu ili hatua dhidi yao zichuliwe na
Tanzania iendelee kuwa moja” alisisitiza Mwenyekiti huyo wa Mkoa wa
Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Aidha Mwanri aliwasisitiza
Wahitimu hao kulinda viapo vyao kwa kuzingatia nidhamu na utiifu kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano na Tanzania na Serikali yake na wananchi kwa
kuwa makini kulinda nchi ili maadui wasiingie nchini na kuaharibu umoja
wa Taifa.
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi
la Kujenga Taifa nchini (JKT) Brigedia Jenerali Elizaphania Marembo
aliwashauri wahitimu wa mafunzo ya JKT kujiepusha na Wanaharakati
watakapokuwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwani wapo ambao lengo
lao ni kuhakikisha nchi inavurugika na Watanzania wanagawanyika.
Alisema kwa wale watakaobahati
kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini ni waende kuwa mabalozi wazuri wa
kuwaelimisha vijana ambao hawakupata fursa ya kujiunga na JKT kuacha
migomo, kutojihusisha na matendo maovu kama vile matumizi ya dawa za
kulevya na vinavyoweza kuwasababisha wapate magonjwa ambayo yanaweza
kuchangia kupoteza ndoto zao.
Kwa wali Mkuu wa Bregedi ya 202
kundi la Vikosi vya Kanda ya Magharibi (FARU) Brigedia Jenerali Stephen
Mkumbo aliwataka wahitimu hao kuwa mabalozi wa masuala ya ulinzi na
usalama katika maeneo yao ili Tanzania iendelee kuwa kisiwa cha amani.
Alisema kuwa kuna baadhi ya
vitendo vyenye viashiria vya ugaidi , hivyo ni vema wakatumia mafunzo
waliopatiwa kuwa vyanzo vya taarifa ambazo ni hatarishi kwa usalama nchi
ya Tanzania na Jeshi lake.
Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la
Kujenga Taifa Msange (823 KJ) Luteni Kanali Mohammed Mketto alisema
kuwa vijana hao wa mujibu wa Sheria waliingia kambi hapo wakiwa 1543 na
wamefanikiwa kumaliza mafunzo yao wote.
Alisema kuwa miongoni mwao
wamefanya usahili wa kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na hivyo
wanasubiri majibu kuingia rasmi katika mafunzo zaidi.
Luteni Kanali Mketto aliongeza
kuwa katika kipindi cha miezi walichokataa wajifunza mambo mengi na
kuweza kufuatua tofauli za kuchoma na kujenga Uwanja ambao utatumika
michezo ya mpira wa kikapu na tenesi.
Akisoma risala ya wahitimu hao
Prisca Mshange alisema kuwa muda unaotolewa kwa mafunzo ni mfupi ni vema
ungaongezwa ili waweze kuelimishwa masomo mengi kuliko ilivyo sasa.
Alisema kuwa baada ya mafunzo
hayo watakwenda kuwa mabalozi wazuri na kuhamasisha shughuli mbalimbali
za kujitegemea na kuwa wazalendo wa kulinda nchi
Kozi ya wanafunzi ilianza juni
12 mwaka huo ambapo wahitimu wameweza kushiriki mafunzo mbalimbali
ikiwemo kujitolea kutoa damu , ujenzi wa uwanja wa mpira kwa ajili ya
mchezo wa pete, mpira wa mikono na kikapu.
SHARE
No comments:
Post a Comment