
Miss Higher Learning Institutions
2016 , Laura Kwai akipunga mkono baada ya kutangazwa kutwaa taji hilo
kwenye Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi
wa pili Evelyn Andrew pamoja na mshindi wa tatu Clara Nyaki.
………………………
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Warembo wa vyuo
vikuu vya Tanzania “Miss Higher Learning Institution 2017” watapanda
jukwaani Septemba 29, kwenye ukumbi wa King Solomoni, Namanga jijini.
Mashindano hayo yameandaliwa na
kampuni ya Glamour Bridal Tanzania baada ya kupewa idhini ya waandaaji
wa Miss Tanzania, Lino International Agency kwa kushirikiana na Baraza
la Sanaa Tanzania (Basata).
Mkurugenzi wa Glamour Bridal
Tanzania Muba Saedo alisema kuwa wanatarajia kufanya mashindano yenye
upinzani wa hali ya juu kutokana na idadi ya vyuo mbalimbali
vilivyothibitisha.
Mbali ya Taasisi ya Ustawi wa
Jamii (ISW), mashindano hayo yatashirikisha vyuo vya Taasisi ya Uhasaibu
Dar es Salaam (TIA), IFM, CBE, UDOM, Tumaini – Makumira na Taasisi ya
Uhasibu wa Arusha (IAA) na Chuo Kikuu Cha Ardhi.
Saedo alivitaja vyuo vingine kuwa
ni Mzumbe, Chuo Kikuu cha Iringa, Tanzania Aviation University College
na Magogoni. Alisema kuwa bado wanapokea maombi kutoka vyuo mbalimbali
na mwisho wa kuthibitisha ni Septemba 11.
“Kwa sasa tunapokea warembo ili
kuweza kushiriki katika mashindano haya, kuna vyuo vilifanya mashindano
na vingine vilifanya uteuzi wa ndani na kutuletea majina kutokana na
kuepuka gharama za kufanya mashindano,”
“Mpaka sasa kuna warembo ambao
wamejitokeza kuwania nafasi tatu za kushiriki mashindano ya Miss
Tanzania mwaka huu, kwa vile tunahitaji mashindano bora yenye ushindani
wa hali ya juu, bado tunawakaribisha wasichana wanaosoma vyuo mbalimbali
kuwasiliana na waandaaji ili kujaribu bahati yao,” alisema Saedo.
Kwa mujibu wa Saedo warembo
wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanatakiwa kuomba kupitia
intagram page higher_learning_miss_tz_2017 au kupitia mubasaedo4me@gmail.com, msaedo@glamourbridal@gmail.co.tz na jmsendo@glamourbridal.co.tz.
SHARE
No comments:
Post a Comment